Thursday, 23 June 2016

Akutwa amekufa msituni




Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
Mwanza. Mkazi wa Kijiji cha Nyangamalila wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza, Mariam Mathias (35), amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha kwenye Msitu wa Buhindi uliopo Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.


Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema, tukio hilo lilitokea Juni 20.
Amesema mwili wa marehemu umekutwa na ukiwa na mikwaruzo kwenye bega la kulia na shingo.
Kamanda Msangi amesema marehemu aliondoka nyumbani kwake Juni 17 mwaka huu kwenda kwenye msitu huo kuchanja kuni, ndipo mauti yalipomkuta.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!