Thursday, 30 June 2016

BABA AUA MTOTO KWA KUMCHAPA NA FIMBO


Picha hii haihusiani na habari husika...



Mwanafunzi wa chekechea Shule ya Awali ya Ilungu, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Julius Leonard (7) amefariki dunia kwa madai ya kuchapwa na fimbo na baba yake wa kambo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu saa 12.00 jioni.


Msangi alisema mtuhumiwa huyo alimuagiza Leonard dukani, lakini alichelewa kurudi hivyo akaamua kumpa kipigo kilichomtoa roho.
“Baada ya polisi kupata taarifa za kuwapo kwa tukio la mtoto kupigwa hadi kufariki dunia, walichukua mwili na kuupeleka kituo cha afya,” alisema Msangi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!