Wednesday, 4 May 2016

WATUMISHI HEWA DAR ES SALAAM WAFIKA 209

Wakati watumishi hewa kwa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongezeka na kufikia 209, wakuu wa idara za mkoa na manispaa wametia saini na kula kiapo kuwabaini bila kuficha ukweli.Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema wamebaini watumishi hewa 209 ambao wameisababishia Serikali hasara ya Sh 2.9 bilioni.

Awali, mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa 17.
Kutokana na ongezeko la watumishi hewa, Makonda aliwaapisha wakuu wa idara za mkoa na manispaa tatu na kuwapa wiki moja kuhakiki iwapo kuna wengine kwenye maeneo yao.
“Awali wakuu wa Idara hao walihakiki watumishi hewa 17 ambao waliingizia (Serikali) hasara ya Sh330 milioni. Baada ya kuwabana maofisa hao tumepata watumishi hewa 209 ambao walilipwa Sh2.9 bilioni, kutokana na hili nimetoa wiki moja wawe wamekamilisha kuhakiki,” alisema Makonda.
Source:Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!