Wednesday, 4 May 2016

Mtoto aliyepewa jezi na Messi ameondoshwa Afghanistan… Baba amekimbia nae

Ni Mtoto kutoka Afghanistan Murtaza Ahmadi ambaye anamkubali sana staa wa soka Lionel Messi na aliamua kuvaa mfuko wa plastiki wenye mfanano na jezi ya Messi kwenye timu ya taifa Argentina ambapo Messi alipoiona ile picha alimtumia jezi mbili kama zawadi na kuziweka saini zake.


_88438940_messi_boy
Stori mpya ni kuwa baba wa mtoto huyu mwenye umri wa miaka mitano amaeamua kuhamia Pakistan na familia yake kutokana na kuhofia maisha ya mtoto wake anayeweza kutekwa au chochote kingine kikatokea sababu baada ya kupewa jezi na Messi wamekua wakipokea vitisho mbalimbali.
Baba wa mtoto huyu amesema siku kadhaa zilizopita alipokea simu nyingi kutoka kwa Wababe waliyedhani Messi katoa hela kwa Murtaza hivyo wanataka mgao wao, hiyo ni moja ya sababu zilizofanya wahame Afghanistan na kwenda kuishi Pakistan ambako Murtaza na wenzake saba wa familia hiyo wanaishi chumba kimoja.
murtaza-ahmadi-lionel-messi
1462266340081

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!