Thursday, 5 May 2016
TUJIFUNZE KUPITIA TUKIO HILI
Kuna mtoto wa miaka nane ameuawa na mama yake kambo maeneo ya Njoro, mjini Moshi karibu na Open university.
Mama wa kambo alikuwa ana miezi takribani minne kwenye ndoa. Alikuwa anampiga sana mtoto na anamnyima chakula.
Siku ya tukio alimpiga mtoto kichwani kwa kisukumio cha chapati. Mtoto alimueleza Baba yake aliporudi jioni maana alikua ana maumivu makali sn. Baba alishikwa na hasira sana akataka kumpiga mkewe lakini mtoto akamwambia "Baba wewe muachie Mungu tu, ila kaninunulie bag la shule, kesho shule"
Kesho yake Baba akaenda kwenye mishemishe zake. Mke akamtumia meseji kwamba "rudi nyumbani kuna dharura" Baba akarudi akamkuta mkewe. Mke akamwambia "namuamsha mwanao lakini haamki"
Kumchunguza mtoto wakakuta amefariki na ametokwa na haja ndogo na kumbwa kitandani.Mama huyu wa kambo akakimbia lakini baadae akajipeleka polisi baada ya wananchi kumtafuta sana. Vipimo vya daktari vimeonyesha kuwa chanzo cha kifo chake ni kupigwa na kitu kichwani.
Pia imebainika utumbo wa mtoto huyo ulikuwa umejikunja kutokana na kukosa Chakula kwa wakati, au kushinda njaa muda mrefu. Mtoto kazikwa jana Moshi.
FUNZO:
Wanaume chunguzeni sana wanawake mnaotaka kuwaoa. Baadhi ni mbwa mwitu wenye ngozi za kondoo. Na nyie wanawake "Jamani mtoto wa mwenzako ni wako, kwanini unamfanyia ukatili kiasi hiki? Huna utu, huna huruma, huna ubinadamu? Ungejisikiaje mwanao angefanyiwa hivyo na mama mwingine?
Wanawake mnatajwa kama watu wenye huruma lakini kuna wakati mnakuwa wakatili kuliko wanyama. Hivi mkoje? Ni mapepo au? Kama humuogopi mumeo wala humheshimu huyo mtoto basi mheshimu Mungu maana hicho ni kiumbe cha Mungu. Pole kwa familia iliyompoteza mtoto huyu.!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment