IKIWA mara yake ya kwanza kushiriki sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Rais John Magufuli ametangaza kupunguza kodi ya mishahara (Lipa Kadri Unavyopata- PAYE) kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa, huku akisema uchumi ukiendelea kuimarika ataboresha pia mishahara ya watumishi.
Hata hivyo, punguzo hilo la asilimia mbili, lililotangazwa jana, litawanufainisha zaidi wafanyakazi wenye mishahara isiyozidi Sh. 360,000, baada ya kukatwa fedha ya kuchangia mfuko wa kijamii.

Aidha, uamuzi huo una maana kwamba serikali itakuwa inapoteza Sh. 3,800 kwa kila mfanyakazi anayelipwa mshahara wa kuanzia Sh. 360,001, Nipashe imebaini.
Akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma jana, Rais Magufuli alitangaza kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 hadi tisa, kuanzia mwaka ujao wa fedha, utakaoanza Julai Mosi, mwaka huu, na kuifanya Tanzania sasa kuwa na tarakimu moja katika kodi hiyo.
Uamuzi huo una maana kwamba mfanyakazi mwenye mshahara unaoanzia Sh. 170,001 hadi Sh. 360,000 (baada ya kukatwa pesa ya mfuko wa kijamii), atanufaika zaidi kwa mujibu wa taratibu zinazotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukata kodi ya PAYE.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mwaka 2008, mfanyakazi mwenye mshahara usiozidi Sh. 170,000 (baada ya kukatwa fedha ya kuchangia mfuko wa kijamii), haukatwi kodi ya PAYE.
Hii ina maana kwamba, mfanyakazi anayelipwa kuanzia Sh. 170,000 hadi 360,000, Paye yake itakuwa asilimia tisa mara kiasi kitakachobaki baada ya kukata Sh. 170,000 isiyolipiwa kodi.
Wafanyakazi wengi wote wenye mishahara inayozidi Sh. 360,000, baada ya kukatwa mchango wa mifuko ya kijamii, watanufaika kwa Sh. 3,800 baada ya kuanza kwa kodi hizo mpya.
MAGUFULI AWEKA WAZI
Akihutubia taifa katika kilele cha Mei Mosi jana, Rais Magufuli alisema licha ya kuwa kumekuwa na ongezeko la mapato serikali, yote hayawezi kuelekezwa kwenye mishahara kwa sababu kuna kundi kubwa la Watanzania wanaotegemea fedha hizo kwa ajili ya kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
“Katika risala yenu (Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania- TUCTA) mmezungumza kupunguza kodi ya mishahara kwa wafanyakazi. Napenda kuwaarifu kwamba serikali yangu imepunguza kodi ya mishahara kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa kuanzia mwaka 2016/17 (mwaka wa fedha). Ni mategemeo yangu wabunge watapitisha bajeti ya serikali yangu.
“Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewapunguzia wafanyakazi mzigo mkubwa. Nimeamua kuanza na hilo ili changamoto za kiuchumi tuzikabili baadaye mambo yakiwa mazuri tutaangalia suala la kupandisha mishahara,” alisema Rais Magufuli.
Alisema tofauti na wafanyakazi, watu wengine kama wafanyabiashara, wao wanaweza kukwepa kodi.
“Wafanyakazi hawa hawawezi kukwepa kodi, wafanyabiashara wanakwepa lakini masikini wafanyakazi hawana njia ya kukwepa ukija mshahara tayari umeshakatwa ndiyo maana nimeamua kupunguza mzigo huu kwao.
“Tutaona mambo yatakavyoenda na kwa hatua hizi kwa mabilioni yanayotumika ovyo kulipa watumishi hewa tutaokoa kiasi kikubwa, tutakaa na Tucta kadri uchumi unavyoenda kuangalia tutakavyoongeza mishaara ya watumishi.
“Katika nchi hii kuna watu wanalipwa mishahara midogo sana na wapo wanaolipwa mishahara mikubwa sana. Leo narudia tena, wale waliokuwa wakipata mishahara mikubwa nimeshasema itakuwa kuanzia Sh. milioni 15 kurudi chini nyingine tupeleke kwa wanaopata mishahara midogo.
“Ndiyo maana kumekuwa na tume ya kupitia mishahara, kumekuwa na wakurugenzi wanahonga wajumbe bodi ili wanapitishe mishahara wanayoitaka wao. Hatuwezi kuendelea hivi, wanaotaka kuacha kazi kwa sababu walizoea mishahara ya Sh. milioni 30 waache kazi.
“Haiwezekani mtu mmoja analipwa Sh. milioni 30 na mwingine Sh. 300,000. Mnapoona tunasimama kupambana na haya mambo mtuombee, lengo letu ni kuona wote wanafaidka na matunda. Hatuonei wivu wale wa mishahara mikubwa… tumeanza kuchukua hatua kuona tunakuwa na mishahara inayozingatia uzito wa kazi kwa kulinganisha ile ya serikali kuu na mashirika ya umma,” alisema Rais Magufuli.
Alisema serikali imeunda bodi za kusimamia mishahara ya watumishi wa sekta binafsi na nyingine ya kusimamia mishahara ya sekta za umma. Pamoja na mambo mengine, alisema bodi hizo zitakuwa na jukumu la kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara.
Alisema wakati wa kampeni zake, aliahidi kuboresha masilahi ya wafanyakazi, “ahadi hii iko palepale, ninapoanza kuchukua hatua hizo ikiwa ni pamoja na kufuta wafanyakazi hewa ni kuelekea kuandaa masilahi bora kwa wafanyakazi wa kweli.
“Ni kweli kabisa kwamba tangu niingie madarakani mapato yameongezeka kwa kubana wakwepa kodi na kupunguza matumizi, siyo dhamira yetu kutumia hela zote kwa mishahara, zinahitajika kwa wengi, huduma bora kwa wananchi zinategemewa, ni sisi kutumia bora rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania wote,” alisema.
WASOMI WACHAMBUA
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Essau Ntabindi, alisema punguzo la PAYE kutoka asilimia 11 hadi tisa, litakuwa na manufaa kwa wafanyakazi wanaolipwa mishahara mikubwa tu.
Alisema kwa wafanyakazi wanaolipwa mishahara midogo hawatanufaika sana, kutokana na kiasi chao kidogo wanachopokea.
Alisema Rais Magufuli amefanya jambo la maana kupunguza PAYE, lakini angeongeza kima cha chini cha mishahara.
Alisema punguzo la asilimia mbili linaweza kufidiwa endapo serikali itaendelea na kasi ya ukusanyaji kodi kwa wafanyabiashara na kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
“Awali watu walikuwa wanakwepa sana kulipa kodi, lakini kwa sasa wamedhibitiwa, hivyo kupunguzwa kwa asilimia mbili kunaweza kukafidiwa,” alisema Ntabindi.
Naye Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema kupungua kwa PAYE ni jambo la msingi kwa maendeleo ya taifa.
Alisema kupungua huko kuendane sambamba na punguzo la gharama za maisha, kama vile kodi za nyumba na gharama za elimu.
“Hata Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kutunga sheria ya kudhibiti kodi za nyumba kwenye Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), mwananchi anashindwa kupanga kutokana na kodi yake kuwa kubwa, hivyo kukiwapo na udhibiti wa kodi za nyumba kutaleta unafuu zaidi,” alisema Ally.
Mchambuzi wa masuala ya Siasa, Abdulhakim Atiki, kwa upande wake alisema punguzo hilo litawanufaisha wafanyakazi wote, lakini wenye mishahara mikubwa ndiyo watakuwa wananufaika zaidi.
Alisema makato ya asilimia 11 ilikuwa kwa wafanyakazi wote na kwamba wafanyakazi wenye mishahara midogo waongezewe.
Atiki alisema wafanyakazi wenye mishahara midogo haiendani na gharama za maisha ya sasa, lakini kupunguzwa kwa asilimia mbili kumedhihirisha kuwa serikali ni sikivu.
Alisema hotuba ya Rais Magufuli imeonyesha serikalini bado kuna uvujaji wa mapato baada ya kubainika watumishi hewa 10,295, hali inayoonyesha Rais anapigana vita ambayo ni ngumu.
TUCTA YAPONGEZA
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya, alisema wamefurahishwa na Rais kupunguza kiwango hicho na kwamba hicho ndicho kimekuwa kilio chao cha muda mrefu.
Alisema punguzo hilo litasaidia kwa kiwango kikubwa kuleta ahueni ya maisha kwa wafanyakazi hao na kwamba kile klilichopunguzwa kitafanya kazi ya kuhudumia mambo mengine.
“Yaani siku ya leo tuna furaha kubwa. Kwa kipindi kirefu huo ndio umekuwa wimbo wetu, lakini tunashukuru serikali hii kutusikia, rais ametukumbuka, na kama ni mtihani tumeshinda asilimia 35 kati ya 100,” alisema.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambaye ni Rais wa TUCTA, Gratian Mukoba, alisema hatua hiyo ya Rais inatakiwa kupongezwa kwa kuwa ameonyesha mwanga kwa wafanyakazi nchini.
Alisema pamoja na kwamba baadhi ya mambo ameahidi kufanyia kazi wanaamini kuwa ni mkweli na hupenda kuzungumza anachokiamini.
Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Haji Semboja, alisema hatua iliyofikiwa na serikali ya awamu ya tano kwa mwanzo ni ishara nzuri.
Alisema punguzo hilo litawanufaisha wafanyakazi wenye ajira rasmi na wenye mikataba, lakini halitawahusu wafanyakazi wanaofanya kazi kama vibarua ambao wanalipwa kulingana na kazi wanayofanya.
Pia, alisema punguzo hilo litaleta faida hasa kwa waajiri kwa sababu sasa wanaweza kuongeza idadi ya wafanyakazi katika makampuni yao kutokana na punguzo hilo.
“Tunaamini kwamba Rais ataziba pengo hili kutokana na vipaumbele vingine, lakini ninashauri kwamba ni vema akakutana na waajiri ili kupanga nao viwango vya mishahara ikiwamo kuhakikisha kwamba hata vile viwanda ambavyo vinatumia watu kama vibarua, vianze sasa kutoa ajira za muda mfupi na mrefu, hiyo itasaidia kuongeza pato la nchi,” alisema.
Imeandaliwa na Sanula Athanas, Fredy Azzah, Gwamaka Alipipi na Elizabeth Zaya
NIPASHE

No comments:
Post a Comment