BAADHI ya viongozi wa dini, wanasaikolojia na vyombo vya dola, wamezungumzia jinamizi la mauaji ya kukatwakatwa kwa mapanga na kuchinjwa, yanayoliandama taifa kwa sasa, ambayo yanadaiwa chanzo kikubwa ni visasi
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, wamesema baadhi ya sababu zinazochangia uwapo wa mauaji hayo ni visasi vinavyotokana na kudhulumiana mali ndani ya familia, mapenzi na uonevu.
Katika kipindi cha mwezi mmoja, watu sita wameuawa kwa kuchinjwa au kukatwakatwa mapanga, chanzo kikidaiwa ni kulipizana visasa.
Tukio la hivi karibuni kabisa ni la mtumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Anethe Msuya (30), aliyeuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana, Kigamboni, Dar es Salaam, lililotokea Mei 26, mwaka huu.
Mei 25, Saidi Simba (mume) na Kadogo Ehicho (mke) waliuwawa kikatili katika Kijiji cha Mmazami, Butiama mkoani Mara kwa kukatwa na mapanga wakiwa wamelala.
Kadhalika, Mei 19, mwaka huu, watu 15 wakiwa wameficha nyuso zao, walivamia msikiti katika mtaa wa Utemini wilayani Nyamagana, Mwanza na kuwaua watu watatu waliokuwa wakifanya ibada usiku kwa kuwakata kwa mapanga na shoka.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa wauaji hao walidai kwamba hatua hiyo imetokana na waumini hao kuendelea na ibada wakati wenzao wanashikiliwa na polisi.
Mei 11, mwaka huu, watu saba wa familia moja waliuwawa wilayani Segerema, Mwanza kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Aidha, Mei 5, mwaka huu, watoto wanne wa familia moja katika kijiji cha Msufini, wilayani Same, Kilimanjaro, waliuwawa kwa kukatwakatwa wakiwa wamelala baada ya kuvamiwa na mtu anayedaiwa kuwa ni ndugu yao.
MALEZI NI TATIZO
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, amesema upotofu maadili unaotokana na malezi hasi ya watoto, umesababisha kuendelea ukatili hadi ndani ya familia.
“Siku zote ukatili usipokemewa utaonekana wa kawaida. Tuheshimu uhai na tujue hatuna mamlaka na uhai wa wanadamu wenzetu. Tusipojenga utamaduni wa kuheshimu haki na utu, matokeo yake ni hayo,”alisema.
Askofu Dk. Shoo alisema ni lazima familia zichukue hatua kufuatilia kwa karibu malezi ya watoto, ikiwa pamoja na kuacha kutenda ukatili kwa kuwa wako watoto wanaokua katika hali ya ukatili kutoka kwa wazazi au walezi na kuona ni jambo la kawaida na wanapotendewa jambo, ulipizi wake ni ukatili na unakuwa mshindi kwa kufanya hayo.
Askofu Shoo alisema tatizo lingine ni vyombo vinavyohusika kutochukua hatua kwa wakati muafaka, kwa kuwa wasipokemea wala sheria kuwabana, ndivyo wanaendelea na kusababisha mauaji.
Alisema dini zote zina wajibu wa kufundisha maadili ili watu wawe na hofu ya Mungu muda wote ikiwa ni pamoja na kuheshimu uhai wa mtu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dk. Leonard Mtaita, alisema wanatarajia kutoa tamko leo kueleza mfululizo wa matukio hayo na kuitaka serikali kuchukua hatua.
Alisema tangu mauaji ya viongozi wa dini yaanze kujitokeza, hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika, kiasi cha kuona kuua ni jambo la kawaida.
“Sasa inaelekea wazi watu wanafanya wazi bila woga. Hakuna aliyekamatwa na kutangazwa hadharana na kuelezwa amehusika na akachukuliwa hatua. Watu hawana woga, wanaona ni jambo la kawaida,” alibainisha.
Aidha, alisema CCT inalaani na kuitaka serikali kuchukua hatua bayana ili kuwafanya watu wawe na woga vinginevyo imekuwa kawaida.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka, alisema: “Tunaangalia changamoto iliyo mbele ya kuwarudisha waumini katika kumjua Mwenyezi Mungu na kujua thamani ya uhai wa mwanadamu. Mwanadamu ni mnyama kama walivyo wanyama wengine, akili iliyojengwa katika imani ya kumwogopa Mwenyezi Mungu ndiyo kidhibiti cha tamaa.”
Alisema udhibiti wa tamaa na ukatili kwa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu humfanya aliyekosewa kuogopa kulipiza kisasi, hivyo hawezi kutenda.
“Ni jukumu la viongozi wa dini kuendelea kutoa mafunzo ili waumini waone kuua ni tendo baya linalomchukiza Mungu, waone uhai ni jambo lenye thamani ambalo Mungu amempa mwanadamu,” aliongeza.
WANASAIKOLOJIA WANASEMAJE?
Grace Makani, Mkurugenzi wa Kampuni ya Masuala ya Kisaikolojia ya Grace Inc. Ltd, alisema mtu anayefikia hatua ya kutokujali na kuua mwenzake kama anachinja ni wazi kuwa amekata tamaa, hana upendo, hana hofu ya Mungu na hajali lolote tena.
“Mwenye familia, malengo na anajua akifanya hivyo atafugwa, hawezi kutekeleza hayo. Wengine wanakuwa na tamaa ya fedha za haraka,” alisema.
Alisema sababu nyingine ni malezi yamepotoka kwa wazazi au walezi kushindwa kutimiza wajibu wao au kuwa sehemu ya ukatili wa kifamilia.
Aidha, alisema ni lazima jamii ijitafakari na kubadilika kwa kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu pamoja na serikali kuangalia namna ya kushughulika ikiwa ni pamoja na namna nzuri ya malezi ya watoto.
Mwanasaikolojia wa taasisi ya Global Source Watch, Dismass Lyassa, alisema mauaji ya aina hiyo yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni tabia ya kuzaliwa, kwamba kuna aina fulani ya ukatili ulifanyika wakati mama ana hali ya ujauzito kwa kuwa asilimia kubwa tabia za binadamu zinabebwa na hali mama akiwa mjamzito.
Sehemu ya pili ni mazingira yanayowazunguka watu wakiwa wameshazaliwa katika umri wa mwaka mmoja hadi sita kama walikuwa wanaangalia picha za kikatili, hujengeka katika akili yao na kuona ni jambo la kawaida.
Lyassa alisema kinachopaswa kufanyika ni wazazi kuwa waangalifu na watoto kama kutoruhusu kwenda kwenye mabanda kuangalia picha za kutisha au kuwa nazo nyumbani
“Unakuta mtu amekudhulumu, amekuwa jeuri, amekujengea mazingira ambayo huwezi kufanya lolote kupata mali zako. Watu wajue kuna watu lazima wakubaliane kabla hawajaanza kama ni biashara, kila kitu kinakwenda kwa maandishi,” alisema.
Alisema kwa mujibu wa jarida la Saikolojia la mwaka jana, mapenzi yanachukua nafasi ya kwanza katika kusababisha mauaji, yakifuatiwa na uchumi.
POLISI WANASEMAJE?
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Diwani Athumani, alisema uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha mauaji mengi nchini ni kulipiza visasi.
Alisema watu wanakuwa na tofauti ya mali katika familia, mirathi, imani za kishirikina, uhalifu wa kawaida kugombani mali na ulevi.
Alisema wanachosahau wanajamii kuwa ziko njia nyingi za kufuata kupata haki, ikiwamo kwenda katika vyombo vya dola na baadaye mahakamani.
“Tuko katikati ya oparehseni. Tunawasaka wote waliohusika na matukio ya hivi karibuni, tunaamini watapatikana. Kabla hawajakamatwa ni vyema wajisalimishe ili kukwepa kuisumbua serikali,” alisema.
Aidha, aliiomba jamii inapoona watu wana nia ovu, wanafanya mambo maovu kabla hayajatokea, waseme, kwa kuwa leo wanaweza kufurahi kwa kuwa aliyepatwa ni mwingine, lakini kesho inaweza kuwa zamu yao

No comments:
Post a Comment