Tuesday, 31 May 2016

Fundi Mabasi Ajinyonga kwa Kuchoka Kuuguaugua!


AJINYONGA (2)
Mwili wa marehemu Charles ldd Ngozoma ukiingizwa kwenye gari la polisi.


Na Dustan Shekidele, UWAZI
MOROGORO: Hali tete! Mtu aliyetajwa kuwa ni Fundi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi ya Al- Jabil ya mkoani hapa, Charles ldd Ngozoma mwishoni mwa wiki iliyopita alitoka nyumbani kwake, Msamvu na kwenda kujinyonga nyumbani kwa mdogo wake, Mwembesongo jirani na Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Usharika wa Bethel Revival Temple, Uwazi lilishuhudia mwili.
AJINYONGA (1)
Mwili wa marehemu ukitolewa ndani ya chumba alichojinyongea huku wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Tukio hilo lililojaza umati kutokana na umaarufu wa marehemu, saa 7 mchana wa Mei 26, mwaka huu nyumbani kwa Rajab ldd Ngozoma  ambaye ni mdogo wake huku kisa kikidaiwa ni marehemu huyo kuchoka kuugua mara kwa mara.
Akizungumza na Uwazi kuhusu madai ya kaka yake kujinyonga nyumbani kwake, Rajab alisema:

AJINYONGA (3)

“Kaka alikuwa akiumwa mara kwa mara na leo kaja kwangu akaniambia kichwa kinamuuma, hivyo nikamnunulie dawa dukani.

“Cha ajabu, niliporeja na dawa, nimemkuta kaka akining’inia, amejinyonga chumbani kwangu.
“Awali alipofika alikuwa ameshika kitu mkononi, inaonekana alishika kamba ambayo ameitumia kujinyongea. Kule kunituma dukani ilikuwa ni njia ya kuniondoa ili apate uwanja mpana wa kujinyonga.”
Kwa upande wake, Mwinyimvua Rajab Ngozoma ambaye ni baba mdogo wa marehemu, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Marehemu ni mtoto wa marehemu kaka yangu, alipofariki dunia baba yake alimuacha mdogo, nikamlea mimi na kumbadilisha dini, kutoka dini ya mama yake ya Kikristo na kuwa Muislam dini ya baba yake. Tulimpa  jina la Ahmed lakini kwa kuwa alisilimu akiwa mtu mzima, jina la Charles ndilo lililozoeleka.
Alipotakiwa kueleza mazingira ya marehemu huyo kujinyonga, alisema:
“Siku za karibuni marehemu alikuwa mgonjwamgonjwa, akachanganyikiwa akili. Ikumbukwe mwanangu alikuwa fundi mkuu wa gereji ya mabasi hivyo baada ya kupata matatizo ya kiafya alipumzika kazi.
“Lakini kwa mshangao jana katoka kwake kaenda kujinyongea kwa mdogo wake.”
Marehemu alizikwa juzi Jumamosi kwenye Makaburi ya Mwembesogo, Morogoro.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!