Thursday, 5 May 2016
BAGAMOYO: Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa kisha kuchinjwa shingoni na watu wasiojulikana eneo la Kaole jana jioni.
Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa kisha kuchinjwa kama kuku maeneo ya Kaole jion ya jana.
Habari kutoka Kaole; Majira ya saa 12 jioni jana, ilipita pikipiki eneo hilo ikiwa imepakiza watu watatu, dereva wa nne! Wanaume wawili, mwanamke na mtoto.
Walipofika eneo la darajani, porini kidogo, pikipiki ilipaki, watu wote wakashuka ndipo hatua za utekelezaji mauaji hayo zilianza.
Inadaiwa kwamba, Mama na mtoto wake walinyongwa Kwanza kabla ya kuchinjwa shingoni mithili ya kuku!
Lakini wakati mauaji hayo yakitekelezwa kulisikika makelele porini ambapo baadhi ya wananchi waliyoyasikia walielekea huko ndipo walipokutana na wauaji hao wakiwa na majambia yaliyoloa damu wakitokea porini.
Walipowaona watu hao walikimbia na kuacha pikipiki yao ambayo inashikiliwa Polisi. Katika eneo la tukio, mbali na pikipiki pia kulikutwa simu tatu za mkononi na mkoba wa mwanamke aliyeuawa.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao ni wageni Kaole na mpaka sasa bado miili yao haijatambuliwa!
Picha zinatisha mno ndio maana hazijatumwa humu kama una ndugu yako mwenye mtoto wa kiume umri miaka 3-5 halafu kapotea mazingira ya kutatanisha jitahidi kufuatilia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment