Monday, 25 April 2016

KIGOGO MBARONI KWA KUHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU NYUMBANI


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani kwake na kuwatumikisha mashambani.


Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia wa kigeni kutenda kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani mwake. Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo, Robert Male.
Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kosa kubwa. Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje kwa dhamana.
Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!