Thursday, 7 April 2016

DK MGAYAWA UDSM ATEKETEA KWA MOTO NDANI YA GARI



Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto akiwa ndani ya gari lake aliyokuwa akisafiria kurejea nyumbani.


Msemaji wa Jumuiya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Kisaka Mussa alisema jana kuwa Dk Mgaya alifariki Jumapili wiki iliyopita asubuhi. “Taarifa tulizonazo ni kwamba alikuwa anatoka mitaa ya Africana kwenda nyumbani, akiwa njiani aligonga lori baada ya muda wakati akiendelea na safari yake, gari yake ilipata moto na kuugua,” alisema Dk Mussa.
Alisema wakati gari yake ikiteketea, Dk Mgaya hakufanikiwa kuokolewa kutokana na moto mkali, hata yeye hakuweza kutoka, hivyo aliteketea akiwa ndani.
“Tulipata taarifa zake kupitia kwenye mitandao ya jamii na baadaye kujiridhisha kupitia namba za gari aliyokuwa akiendesha,” alisema Dk Mussa.
Taarifa zilizosambazwa mitandaoni zikimkariri Mkuu wa Idara hiyo, Dk Honest Kimaro akisema kuwa kabla Dk Mgaya alipata ajali iliyosababisha gari lake kuteketea moto akiwamo ndani. “Kwa ujumla tumeshtushwa sana na msiba huu. Dk Mgaya alijiunga na idara yetu miaka minne hivi iliyopita akitokea masomoni Marekani,” inasomeka taarifa hiyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!