Dawa hizo za malaria aina ya Amoxycillin na Septrine pamoja na vipodozi vyenye thamani ya Sh150 milioni zimekamatwa na polisi waliokuwa doria katika Mji wa Buseresere wilayani hapa, zikisubiri kuingizwa sokoni.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wilaya ya Chato, Abdallah Mtumwa amesema shehena ya dawa na vipodozi ilikutwa kwenye gari aina ya Fuso.
“Askari wa Kituo cha Polisi cha Buserere walikamata shehena hiyo baada ya kuingizwa hapa nchini kutokea nchi jirani ya Uganda kwa njia ya magendo,” amesema.
Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda Ziwa, Aggrey Muhabuki amesema bidhaa hizo hazina usajili wa kuingizwa nchini.
MWANANCHI.
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment