Thursday 17 March 2016
WAZIRI AWATAKA WAPIGA DEBE WAONDOLEWE DAR
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize kwenye shughuli za ufanyaji kazi,
Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya kihalifu. Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,
Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,
“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.
Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment