Wednesday 16 March 2016

WAFUGAJI KUANZA KUFUGA KWA VITARU( KISASA) BADALA YA KIHOLELA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja wadume
la ng’ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9 shamba
la kitengule-Karagwe.


Baadhi ya ng’ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule ambapo kwenye
block hii moja kuna Ng’ombe zaidi ya 800 wanaolishwa na kuhudumiwa
vizuri na mmiliki wa kitaru hiki
.Ng’ombe wakitoka kuogeshwa kwaajili ya kuua baadhi ya wadudu kama kupe
wanaopendelea kukaa kwenye mwili wa ng’ombe.Hili ni moja ya josho la
kisasa ndani ya kitaru namba 9.
Kufuatia ziara ya waziri mkuu,Mh:Kassim Majaliwa ndani ya mkoa wa Kagera akiwa
ameambatana na waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu Waziri
wa Mambo ya ndani,Ziara hiyo imekuja na maagizo kadhaa ikiwamo wamiliki
wote wa vitaru kwenye ranchi za Taifa ambao hawajaziendeleza waziachie
mara moja na maeneo hayo yagawiwe upya,Waziri Mkuu ameagiza pia kwa
wamiliki wa vitaaru ambao sio watanzania wajisalimishe au waondoke
kwenye vitaru hivyo kabla hatua kali hazijaanza kuchukuliwa.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na timu yake ya
wataalamu wameshaanza kupitia vitaru vyote “blocks” na wamiliki wake
ikiwepo pia idadinya mifugo kwa kila block,Hii leo Mwigulu Ncheba
amekutana na wamiliki wa vitaru kwenye shamba la Kitangile-Karagwe na
kuagiza wamiliki wote ambao hawajaendeleza maeneo wanayoyamiliki
yanachukuliwa na serikali kwaajili ya kuwapatia watanzania wenye uwezo
wa kuziendesha.
Mwigulu Nchemba ameagiza pia wamiliki wa vitaru kuacha mchezo wa kukodisha na
kuingiza mifugo kutoka kwa wafugaji haramu wa nchi jirani,kitendo hicho
ni kosa na yeyote atakayebainika anakwenda jela na adhabu kali itafuta.
Mbali na vitaru hivyo,Waziri Mkuu akishirikiana na waziri wa kilimo wameagiza
ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera kuondoa wavamizi wote kwenye pori
tengefu ya serikali kabla hatua zingine zinazofuata kuanza kutekelezwa.
Kupitia uwekezaji mzuri kwenye kitaru namba 9 cha shamba la Kitengule,Mwigulu
Nchemba ametoa rai kwa wafugaji wote nchini kuanza kujipanga kufuga kwa
mfumo wa vitaru ili kuachana na ufugaji holela unaopelekea migogoro
mbalimbali na wakulima.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!