Saturday 26 March 2016

Picha za Ajali iliyotokea Kimara Dar es salaam usiku wa March 25

Ikiwa zimepita wiki mbili tangu kutokea kwa ajali  Kimara Dar es salaam, Usiku wa kuamkia March 25 kumetokea ajali nyingine Kimara Baruti ambapo basi la Princes Murolenye usajili namba T 551 BQP limevamia kituo kipya cha abiria.


Taarifa rasmi zinasema kuwa basi hilo lilokuwa likitokea Arusha kuja Dar es salaam halikuwa na abiria wala hakuna aliyefariki, kwa mujibu wa mhusika wa basi hilo alisema, basi hilo lilipopata itilafu maeneo ya mto Wami wahusika  walichukua uamuzi wa kuwaamisha  abiria wote kutoka kwenye basi hilo na kuwapeleka kwenye basi lingine kwahiyo mpaka linaingia Dar na kupata ajali halikuwa na abiria.
.
.
.
.
PICHA KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!