Sunday, 20 March 2016

Moja kwa Moja: Uchaguzi wa marudio Zanzibar

07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja.
Shein
Image captionDkt Shein akioneasha wino kwenye kidole chake
07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa.


06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo. Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri.
06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe.
06:35 Katika vituo vingi, wapiga kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.
06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani Zanzibar wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi. Chama cha CUF kinasusia uchaguzi huo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi huo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!