Wednesday, 10 February 2016

Safari ya Yanga Mauritius iliyopangwa leo, yakwama

Yanga ilitarajiwa kuondoka hii leo lakini ndege waliyokuwa wakitarajia kuondoka nayo haikuwa na nafasi kwa wachezaji wote hivyo wangetakiwa kujigawa lakini kwa kuwa wanahitaji kuondoka pamoja wameamua kusubiri ndege ya kesho ambayo ina nafasi ya kutosha kuondoka na kikosi kizima.


Yanga itacheza mchezo wa kwanza wa Raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim siku ya Jumamosi ya Febuari 13 mwaka huu.
Kikosi hicho kitaondoka na idadi ileile na kuwaacha wachezaji wake watatu kama ilivyopangwa hapo awali ambao ni Mlinda mlango Benedicto Tinocco, kiungo Godfrey Mwashiuya na mshambuliaji Matheo Anthony huku wachezaji waliokuwa majeruhi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Amissi Tambwe wote wakisafiri na timu.
Mkuu wa msafara ni Ayoub Nyenzi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati upande wa viongozi wanakwenda Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro.
Wachezaji watakaooondoka ni
Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
Mabeki; Juma Abdul, Mbuyu Twite (DRC), Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Pato Ngonyani.
Viungo ni; Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Issoufou Boubacar (Niger) na Deus Kaseke.
Washambuliaji ni; Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe).
Benchi la Ufundi litakuwa na
Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi)
Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi
Kocha wa Makipa; Juma Pondamali
Daktari; Nassor Matuzya
Meneja; Hafidh Saleh
Mchua Misuli; Jacob Onyango
Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!