Wednesday, 10 February 2016

IGP: WATU BINAFSI WANYANG'ANYWE SILAHA


Jeshi la Polisi nchini linaangalia uwezekano wa kukusanya na kuzichunguza silaha zote zinazomilikiwa na watu binafsi kwa lengo la kupambana na uhalifu hususan ujangili.

Sambamba na hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amesema wameunda kikosi kazi cha kupambana na ujangili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, kutokana na  kushambuliwa kwa helikopta ya doria na kuuawa kwa rubani  Rogers Gower, Januari 29, mwaka huu, huku juzi Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, akikamatwa kwa madai ya utunguaji chopa hiyo.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kudhibiti matumizi mabaya ya  silaha ambazo zinatolewa kwa wananchi kihalali na kwamba baada ya kuzikusanya watazifanyia uchunguzi kwa kuangalia matumizi yake.
“Unaponunua silaha lazima upewe na risasi, kama ulinunua risasi 100 halafu tukakuta una risasi 20, hizo 80 utatueleza matumizi yake. Kama ulizitoa kwa majangili tutajua tu na kama ulikwenda kuwindia lazima utuonyeshe kibali cha uwindaji,” alisema.
Mangu alisema uchunguzi wao umebaini kuwa wananchi wengi wanaoishi kando ya hifadhi ya taifa na wale wanaomiliki silaha hizo, wanawaazimisha majangili na kwenda kufanyia uhalifu. 
Alisema katika uchunguzi huo wapo ambao watanyang’anywa na wengine watapewa utaratibu wa kuzitumia kwa kuwa lengo la kufanya hivyo ni  kudhibiti matumizi mabaya ya silaha hizo.
Alisema kwa sasa uaminifu umepotea kwa watumiaji wa silaha kwa kuwa watu badala ya kuzitumia kwa kujilinda, wanazikodisha kwa majangili wanaomaliza wanyamapori.
kia mahali tukafuta kutoa silaha au tukatengeneza utaratibu kwa idara ya wanyamapori wakapewa bunduki na wale wanaotaka kwenda kuwinda kuomba kibali watapewa na silaha ya kuwinda  kwa muda wa siku chache na kuzirudisha, tutaangalia huko mbele tutafanya nini,” alisema
Naye Prof. Maghembe alisema wanakamilisha haraka uanzishaji wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa wanyamampori.
Alisema kikosi hicho kitaundwa kwa kushirikisha taasisi zote za Wizara ambazo ni Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). 

NIPASHE.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!