skip to main |
skip to sidebar
CHAKULA CHA MTOTO: VIAZI LISHE, KAROTI NA MAZIWA
Mahitaji
- Viazi lishe 2
- Karoti 2 kubwa
- Butter (salted)kijiko kimoja cha chai
- Maziwa robo lita
Maelekezo
- Menya viazi na karoti. Kata vipande vidogo sana.
- Weka viazi na karoti kwenye sufuria, ongeza butter kisha bandika jikoni.
- Baada ya dakika 20, vitakua vimeiva. Epua acha vipoe kidogo.
- Weka kwenye blender,ongeza maziwa kisha saga. Hakikisha chakula kimelainika kabisa mtoto wa miezi 6 anaweza kula.
- Toa muwekee mtoto kwenye bakuli mlishe.
No comments:
Post a Comment