Thursday 14 January 2016

MKATE WA ZUCCHINI NA KOROSHO



Kuandaa: dakika 20 
Mapishi: dakika 55


Mahitaji

  • Mayai 3
  • Butter kikombe 1 iyeyushe
  • Sukari vikombe 2
  • Zucchini vikombe viwili (lipo kama tango ila siyo tango)
  • Vanila vijiko 2 na nusu vya chai
  • Unga vikombe 2
  • Mdalasini vijiko 3
  • Baking soda kijiko 1 cha chai
  • Baking powder robo kijiko cha chai
  • Chumvi nusu kijiko cha chai
  • Korosho nusu kikombe vitwange au visage zivunjike vunjike ila unaweza tumia pia njugu, karanga, yaani jamii yoyote hata matunda ukitaka.
  • Nutmeg kijiko 1 chai

Maelekezo

  • Pasha oven nyuzi joto 200, kuchukoa chombo utakacho okea mkate kipake butter, hakikisha chote kimeenea mafuta kisha weka unga kidogo usambaze. Kiweke pembeni.
  • Chukua zucchini, lioshe usilimenye kisha likwangue kwa kutumia kifaa cha kukwangulia karoti.
  • Chukua bakuli, pasua mayai koroga,weka butter na sukari koroga mpaka sukari ilainike, weka zucchini na vanila endelea kukoroga kisha weka pembeni.
  • Chukua unga weka mdalasini, nutmeg, baking soda, baking powder, chumvi na korosho.
  • Changanya kwenye mchanganyiko wa kwanza. koroga mpaka uhakikishe vimechanganyikana vizuri vyote.
  • Mimina kwenye chombo ulichokipaka mafuta na unga. Kisha weka kwenye oven na oka kwa dakika 40 mpaka 50, utoe upoe anza kujiramba na familia.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!