Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) akiwatangazia wananchi na wanahabari dakika chache zilizopita mara baaada ya Mahakama Kuu ya Ardhi kusogeza mbele usikilizwaji wa kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa kwa nyumba za Mabondeni hasa zile zilizopo kwenye bonde la jimbo hilo la Kinondoni kesi iliyofunguliwa na mbunge huyo kutetea wanachi wake ikiwemo wapatiwe haki za msingi hasa maeneo mbadala na salama. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Andrew Chale, Modewjiblog
Kesi ya msingi ya kupinga Ubomoaji wa nyumba zilizopo kwenye mabonde ya wakazi wa jimbo la Kinondoni iliyofunguliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Maulid Mtulya (CUF) ambayo inataka wananchi hao mbali na kubomolewa wapewe maeneo mbadala na yenye usalama, iliyofunguliwa Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi, jijini Dar es Salaam, imesogezwa mbele hadi hapo 25 Januari itakapotolewa hukumu.
Akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari, Mbunge huyo, amebainisha kuwa, baada ya leo Januari 14, kufika mahakamani hapo na pande zote kuendelea na mashahuriano, ikiwemo Mbunge huyo la kuweka zuio la muda la kutobomolewa kwa nyumba zote za Mabondeni ndani ya jimbo la Kinondoni, Hata hivyo waendesha kesi wamesogeza mbele hadi hapo 25 Januari, majira ya saa nane mchana itakapotolewa mahamuzi kamili.
Awali nje ya mahakama hiyo iliyopo katikak jengo la Shirika la Nyumba eneo la Posta, ilijaa na umati mkubwa wa wananchi wa mabondeni wakiwemo wale waliobomolewa nyumba zao pamoja na waliowekewa alama nyekundu ya X, wakisubiria hukumu hiyo.
Hata hivyo baada ya kuharishwa kwa kesi hiyo, wananchi hao walitoa dukuduku lao kwa Serikali kuchukua hatua ya haraka kumaliza hilikujua hatima yao.
Mkazi wa mabondeni, Riziwan Mtambo akizungumza na wanahabari baada ya kesi yao hiyo kusogezwa mbele huku akidai kuwa Serikali inawazunguka kwa kushindwa kutoa jibu la msingi iliwajue wanachukua hatua gani.
Mmoja wa wakazi wa mabondeni akizungumza na wanahabari akielezea namna wanavyopata taabu kila kufika Mahakamani hapo bila kupatiwa jibu la uhakika. Ambapo aliomba hukumu ya kesi hiyo kutolewa jibu haraka.
Wakazi hao wakimsikiliza Mbunge wao, Maulid Mtulya (hayupo pichani) wakati wa kutolewa ufafanuzi wa mwenendo wa kesi yao hiyo iliyosogezwa hadi hapo 25 Januari.
Wakazi hao wa mabondeni wanaofiuatilia kesi yao ya msingi wakionekana wakiwa nje ya viunga vya Mahakama hiyo ya ardhi wakisubiria hukumu ambayo hata hivyo imesogezwa mbele hadi hapo 25 Januari.
No comments:
Post a Comment