Saturday, 30 January 2016

Mapishi ya leo: Sweet, Sticky and Spicy Chicken!




Kuandaa: dakika 15 
Mapishi: dakika 30


Mahitaji

  • Kuku nusu kilo
  • Asali vijiko 4
  • Sukari ya brown  kijiko 1 na nusu
  • Soy sauce nusu kikombe ,hii ni sawa na vijiko 8 vya mezani
  • Tangawizi vijiko 2 vya chai
  • Kitunguu saumu vijiko 2 vya chai
  • Chilli sauce vijiko 3 vya mezani
  • Chumvi kiasi
  • Cayenne pepper kiasi
  • Mafuta ya olive vijiko 5 vya chakula
  • Currypowder kijiko 1 cha chai
  • Coriander powder kijiko 1 cha chai
  • Ndimu 1

Maelekezo

Mapishi haya ya kuku yanakupa nafasi ya kuona ubora wa mapishi kwa mlo wa muda wowote unaopendelea. Unaweza kula chakula hiki asubuhi, mchana au jioni. Ndio ubora wa kuku aliyepikwa kwa staili hii.
  • Changanya pamoja sukari, asali, soy sauce, tamgawizi, kitunguu saumu na chilli sauce kwenye kibakuli kidogo.
  • Safisha kuku, mkaushe maji, mkate vipande vidogo vidogo muweke kwenye kikaangio, mnyunyizie chumvi, cayenne pepper na ndimu kiasi.
  • Weka mafuta jikoni kisha weka kuku na anza kumgeuza gueze kuku mpaka mafuta yapate moto, usiache kugeuza mpaka kuku awe wa brown.
  • Weka viungo vilivyobaki currypowder na coriander powder, koroga kwa dakika 5.
  • Mwisho mwagia sauce uliyoandaa, usifunike. Pika hadi sauce iwe nzito.
  • Epua nyama ya kuku na jirambe na familia.


Asante kwa  Misosi .com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!