Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na aliyekuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamadi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Januari 11, 2016 katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusiana na suala la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba (kushoto), Mwenyekiti wa Mambo ya Siasa wa chama hicho,Twaha Issa, Kulia ni Mshauri wa Mambo ya Siasa wa Chama hicho Bw. Mansour Yusuf.
Maalim Seif amesema kuwa hana taarifa zozote juu ya swala la kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake ametaka kura zilizobaki zihesabiwe na mshindi aweze kutangazwa.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mstaafu Jecha Salum Jecha alikuwa hana mamlaka ya kufuta uchaguzi kutokana na hatua zote za uchaguzi.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi bila kuwa na wajumbe walio wengi wanaounga mkono kile wanachotaka kuamua, hali ambayo haikufanyika wakati wa kufuta uchaguzi huo.
Waandishi habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea kumsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
No comments:
Post a Comment