TANZANIA imeanza kuathirika na kushuka kwa bei ya mafuta duniani katika uwekezaji wa mafuta na gesi kwa kupungua shughuli za utafutaji mafuta kutoka kampuni 25 hadi nusu ya idadi hiyo.
Pia katika mikoa ya Lindi na Mtwara viwanja vimeanza kupungua bei pamoja na hoteli kukosa wageni, tofauti na ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Mataragio alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uelewa wa sekta ya mafuta na gesi nchini.
Dk Mataragio alisema, kutokana na kushuka bei ya mafuta duniani kwa miaka miwili iliyopita kutoka dola milioni 120 kwa pipa hadi dola 28 kwa pipa na Tanzania ikiwa mshiriki katika sekta hiyo, athari zimeanza kuonekana.
No comments:
Post a Comment