Sunday, 31 January 2016
ISMAIL MUSSA NA SIRI YA MAPENZI!
Mapenzi ni vile wewe unataka yawe, mapenzi hayaoti kama uyoga,
ila mapenzi ni shamba ambalo linahitaki kila siku kupaliliwa,
mwisho wa siku litoe mavuno ambayo yameendelea.
Kila siku penzi linatakiwa kupaliliwa kwa upendo, heshima na kujali na neno samahini ni kama jembe la kutoa magugu yaliyouzunguka mmea wa mapenzi na kutoa msamaha ni kipimo cha upendo wa dhati kwa yule unayempenda.
Mpenzi wa kweli ni yule anayechukua matatizo yako na kuyafanya kuwa yake, aliyetayari kupambana kwa ajili yako, aliyetayari kuteseka kwa ajili yako, aliyetayari kupoteza ili wewe upate, na aliyetayari kusimama kwa niaba yako ili uwe mshindi
Ukweli na uaminifu ndio nguzo pekee ya kusimamisha mnara wa penzi lako, ukiwa mkweli utakuwa mwaminifu na ukiwa mwaminifu utakuwa mkweli
Mapenzi hayana mjuzi wala mapenzi hayana fundi ila dawa ya mapenzi ni kuridhika na yule unayempenda na kuamini hakuna zaidi yake.
Mpende anayekupenda, mheshimu anayekuheshimu na mjali anayekujali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment