Wednesday 30 December 2015

SERIKALI KUIWABANA MADAKTARI INAOWASOMESA NJE YA NCHI.

Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya
Shinyanga. Serikali imesema madaktari wote watakaopata nafasi ya kusoma nje ya nchi kwa ufadhili wake, watafanya hivyo kwa kusaini mkataba.


Kufanya hivyo kumeelezewa kuwa kutasaidia kuwabana wale wanaohitimu na kutimkia nje ya nchi kwenda kufanya kazi huko.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalah alipotembelea Manispaa ya Shinyanga.
Alisema Serikali imeendelea kuwapoteza madaktari wengi inaowasomesha wanaokimbia kwa madai ya mazingira mabovu ya kufanyia kazi.
Wengi wao hukimbilia nchi za Afrika Kusini na Botswana wanakodai kuna mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Alisema wanataka kuona wizara inakuwa na madaktari bingwa wa kutosha kulika ilivyo sasa.
Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Fredrick Mlekwa alimwambia naibu waziri huyo kuwa, tatizo kubwa linalokwamisha utendaji kazi wao ni upungufu wa madaktari hospitali hapo.
Dk Mlekwa alisema hospitali hiyo ina madaktari bingwa wanne, madaktari wa kawaida 15 na madaktari wasaidizi kumi na moja. Alisema kwa mwaka hutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 500,000.

MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!