Tuesday 1 December 2015

PAPA FRANCIS. WAISLAM NA WAKRISTO NI NDUGU"

Papa Francis amewaambia waumini kwenye msikiti katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati “Wakristo na Waislamu ni ndugu”.


Alikuwa akizungumza na Waislamu ambao walipewa makazi Bangui kufuatia miaka takribani mitatu ya vita baina ya Wakristo na Waislamu.
Ziara ya msikitini ilionekana kama sehemu isiyowezekana katika ziara ya Afrika, alisema mwandishi wa BBC.
Papa Francis atahitimisha ziara yake ya Afrika na wananchi mjini Bangui.
Waislamu wengi waliondoka katika mji mkuu kufuatia mapigano na kubaki wengine 15,000 katika eneo linaloitwa PK5, ambalo lilizungukwa na wanamgambo wa Kikristo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!