Tuesday 1 December 2015

HATIMAYE MWILI WA MAWAZO WAZIKWA GEITA



1
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kwa majonzi makubwa akiweka udongo kwanye kaburi la kamanda wake Alphonce Mawazo. Katikati ni waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mh. Fredrick Sumaye.


2
Mtoto wa marehemu Precious Alphonce Mawazo akifatana na Godbless Lema kuweka udogo kwenye kaburi la baba yake wakati wa kumuifadhi kijijini kwao Chikobe.
3
Mhe. Edward Lowassa akiweka udongo kwenye kaburi la aliyekuwa M/kiti na mgombea ubunge Jimbo la Busanda kamanda Alphonce Mawazo kijijini kwao Chikobe.
4
Mwili wa kamanda Mawazo ukitumbukizwa kwenye nyumba yake ya milele kijijini kwao Chikobe.
5
Mhe. Edward Lowassa (katikati), Fredick Sumaye (Kushoto) mtoto wa marehemu Precious Mawazo ( Kulia) wakiwa katika eneo la makuburini ambapo mwili wa kamanda Mawazo ullipokuwa unaifadhiwa.
6
Mtoto wa marehemu Precious Mawazo akimuaga baba yake kwa simanzi nzito.
7
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA), Mh. Edward Lowassa akiwasili msibani.
8
Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh. Freeman Mbowe naye akiwasili katika eneo la kumuaga marehemu Mawazo.
9
Ndugu wa marehemu wakiaga mwili wa Mawazo.
Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh. Freeman Mbowe jana ameongoza mamia ya wakazi wa Mkoa wa Geita katika mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Alphonce Mawazo yaliyofanyika kijijini kwao Chikobe wilayani Geita.
Mazishi hayo yalitanguliwa na waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho katika uwanja wa kijiji cha Chikobe licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kuanzia majira ya asubuhi.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA), Mh. Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mh. Fredrick Sumaye, makamu mwenyekiti wa Chadema upande wa Zanzibar Said Issa Mohamed na kaimu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu.
Kabla ya mazishi kufanyika, Mh. Mbowe aliwapa neno la faraja wafiwa.
Ilipotimu majira ya saa tisa na dakika ishirini na moja alasiri jeneza lililoubeba mwili wa marehemu Alphonce Mawazo likashushwa kaburini na vijana wa kikosi cha ulinzi wa Chadema maarufu kama Red Brigade ikiwa ni siku ya kumi na saba toka alipouawa kikatili kwa kukatwa na mapanga.

PICHA KWA HISANI YA GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!