Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 35
- Prawns kilo 1
- Pilipili manga vijiko 2 vya chakula
- Kitunguu saumu 2
- Tangawizi kijiko 2 iliyosagwa
- Oyster sauce kikombe 1 cha kahawa
- Olive oil kikombe 1 cha kahawa
- Chumvi
- Ndimu 1
- Cayenne pepper kijiko 1 cha chai
- Paprika kijiko 1 cha chai
- Thyme kijiko 1 cha chakula
- Mustard powder kijiko 1 cha chakula
- Oregano kijiko 1 cha chai
Maelekezo
- Chukua prawns, wasafishe vizuri. Wakamulie ndimu watie na chumvi. Waweke pembeni.
- Chukua bakuli weka olive oil na viungo vyote. Changanya vizuri sana.
- Chukua prawns, waweke kwenye ule mchanganyiko hakikisha wameendea viungo.
- Hakikisha prawns wameenea viungo vizuri.
- Funika bakuli vizuri au weka kwenye mfuko kisha waweke kwenye fridge.
- Acha wakae usiku mzima, au masaa 5. Chukua wavu wakuokea upake mafuta
- Uweke jikoni ukipata moto panga prawns kua unawageuza baada ya dakikia 5, ukimgeuza unampaka ile sauce ya viungo.
No comments:
Post a Comment