Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri.
Magufuli amesema baraza nitakalolichagua halitakuwa na semina elekezi, kama ni semina watajipa huko huko ndani, wenyewe. Baadhi ya Wizara na Mawaziri wake, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora ni Simbachawene naibu wake ni Angela Kairuki.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano hajapatikana na Naibu ni Edwin Ngonyani. Waziri ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu ni Jenesta Mhagama Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki ni Balozi Augustino Mahiga, naibu wake ni Dk. Suzan Kolimba.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni William Lukuvi Wizara ya Elimu Waziri bado hajapatikana, Naibu Stella Manyanya Waziri wa Afya Jinsia na Watoto ni Ummy Mwalimu, Naibu wake ni Dk Hamis Kigwangalla Waziri wa Nishati na Madini ni Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Katiba na Sheria ni Dk Harison Mwakyembe na Maziri wa Ulinzi ni Hussein Mwinyi.
Waziri wa Habari na Michezo ni Nape Nnauye. Baadhi ya wizara bado hazijapata mawaziri ingawa zimepata manaibu mawaziri ikiwemo Wizara ya Fedha.
No comments:
Post a Comment