Thursday, 17 December 2015

JE WAFAHAMU HISTORIA YA MJI WA TANGA?




Mkoa wa Tanga una ukubwa wa eneo lenye kuwa na  kilomita za mraba 27,348  ambayo ni sawa na takribani asilimia 3 ya ukubwa wa  jumla ya nchi nzima yenye ukubwa wa kilomita za mraba 945,202. 

Idadi ya jumla ya wakazi wananchi watanzania wa mkoa wa Tanga karibia ni millioni 2  wakati ambapo manispaa ya mji wa Tanga mjini idadi ya wakazi wananchi inakaribia zaidi ya laki tatu.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI MKOANI TANGA
Wakazi wananchi walio wengi kama jinsi ilivyo katika mikoa mingineyo Tanzania ,katika mkoa wa Tanga wanapatikana wakiishi katika maeneo ya vijijini(mashambani )ambao hujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo.



Katika wakazi wananchi wanaopatikana wakiishi katika maeneo ya mwambao wa pwani kawaida hujishughulisha na uvuvi wa samaki pamoja na biashara ndogondogo.


Wengineo hujishughulisha na biashara kubwa na za kati,utengenezaji wa ngalawa na mitumbwi,utengenezaji wa mikaa pamoja na chumvi.


Ikumbukwe na ifahamike ya kwamba mkoa wa Tanga ndio mkoa pekee nchini kuwa na Bandari ya Tanga ambayo ni ya pili kwa ukubwa  baada ya bandari ya Dares-salaam.
FURSA ZA KIUCHUMI NA KIUTALII ZIPATIKANAZO MKOANI TANGA.
Ni pamoja na ukanda mrefu wa mwambao wa pwani yenye kuwa na mandhari nzuri zenye kupendeza kama vile ghuba,matumbawe,ghuba za kwale,manza,moa,Tanga pamoja na mwambani.

 
Fukwe zipatikanazo mkoani Tanga ni pamoja na kigombe,pangani na ushongo.Fukwe hizi zimefunikwa na kuzungukwa na aina mbalimbali za visiwa kadhaa kama vile ulenge na toten ambavyo vinatoa fursa kadhaa za kiutalii na malazi.



Maeneo yenye kuwa na mandhari nzuri na mvuto katika kutembelea uwapo mkoani Tanga ni pamoja na mji wa kihistoria mjini Tanga, visiwa vya Toten,ulenge ,Yambe,Karange,maziwe pamoja na pangani iliyo karibu kabisa na mapango ya Amboni. 

Maeneo mingineyo ni pamoja na magofu ya kale ya  Tongoni na maji moto ya Gallanos.
MAENEO YA UHIFADHI YAPATIKANAYO MKOANI TANGA :
Mkoa wa Tanga umebarikiwa kwa kuwa na maeneo ya uhifadhi wa mali asili (protected areas)kama vile mapori ya akiba ya wanyamapori  na maeneo ya hifadhi za Taifa(National parks). 



 Maeneo haya ya uhifadhi ni pamoja na Hifadhi za Taifa za saadani na mkomazi,msitu wa asili wa Amani (Amani nature reserves na hali kadhalika maeneo ya uhifadhi ya baharini ya visiwa vya maziwe.


Mkoa wa Tanga vilevile una uoto wa asili wa mimea ya miti ya misitu ya mikoko,maeneo yenye ardhi nusu jangwa ya uoto asili wa  miti ya misitu katika ardhi katika mwambao wa pwani ya Afrika ya mashariki.

Misitu ya mvua ya ukanda wa nchi za joto ni moja ya mazingira ya makazi ya patikanayo mkoani Tanga katika milima ya usambara zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari ambayo mazingira haya ya makazi ni moja ya sehemu muhimu ya uoto wa asili bainuai kimataifa.


Milima ya Tao la mashariki (Eastern arc mountains)yenye kuwa na utajiri wa asili wa mimea na wanyamapori vinapatikana kwa wingi katika safu ya milima hii.
 


Vivutio vinginevyo vya kiutalii mkoani Tanga ni pamoja na makazi ya wamaasai na wapare katika wilaya za Handeni na Korogwe na bila kusahau mashamba maarufu ya zao la kibiashara la Mkonge.
MAJENGO YA KIHISTORIA YA KALE MKOANI TANGA.
Mkoa wa Tanga umebarikiwa kwa kuwa na majengo ya kihistoria ya kale tangu enzi  za ukoloni wa kijerumani(kati ya mwaka  1881 mpaka 1916 mpaka 1961)na vilevile waingereza kati ya miaka 1916 mpaka 1961.

HISTORIA YAKE FUPI YA MKOA WA TANGA;
Mkoa wa Tanga ni moja ya miji mikongwe inayopatikana  katika pwani ya Afrika ya mashariki ya mwambao wa pwani.


Kihistoria tangu enzi za kikoloni na wavumbuzi kama vile
Vasco-Dagama,Waarabu,Wajerumani,Waingerezapamoja na wageni mbalimbali kutoka mataifa ya kigeni,biashara ya watumwa mpaka leo hii inaufanya mkoa huu kuwa na upekee wa utajiri wa kihistoria nchini Tanzania

Neno ‘Tanga’ maana yake ni ‘elea’katika lugha ya Kiswahili ikimaanisha ya kwamba mwambao wa ghuba ya Tanga katika karne nyingi umesaidia kutoa huduma salama za kiuchumi kwa wavuvi pamoja na biashara nyinginezo zipatikanazo katika mwambao wa bahari ya hindi katika pwani ya Afrika ya mashariki.

Lakini vilevile neno Tanga maana yake nyingine katika lugha ya kabila la wabondei inamaanisha ‘SHAMBA’.
Mji wa Tanga pamoja na pangani ilikuwa ni miji muhimu sana kama vituo vya biashara ya watumwa na meno ya tembo au ndovu na pale wakati sultani wa maskati na omani alipohamia Zanzibari katika miaka ya 1832 na mara moja ilipelekea sultani huyu kuanza kudhibiti na kutawala eneo lote la ukanda wa pwani ya Afrika ya mashariki takribani maili 10 hivi.
Ilipofikia wakati wa kuligawa bara la Afrika katika kipindi cha miaka ya karne ya 19, Maslahi ya kibiashara na kiuchumi yalipekea wajerumani kununua na kuchukua ukanda wa mwambao wa pwani kutoka kwa sultani na kuendeleza koloni la ujerumani la Afrika ya mashariki.  


Hivyo basi hali hii ilipelekea wajerumani kubakia na bandari yao ya Tanga pamoja na ardhi nzuri yenye kuwa na rutuba hasahasa katika maeneoya milima  ya Usambara na hatimaye ikaifanya Tanga kuwa kituo muhimu cha serikali ya kikoloni cha wajerumani toka miaka ya 1890 mpaka pale ilipofikia mji wa Dares salaam kufanywa kuwa mji mkuu wa kibiashara na kiuchumi.
Haraka haraka miundo mbinu ya watawala  wajerumani ilianzishwa pamoja na maendeleo ya kiuchumi ilifuatiwa katika miaka ya 1889 baada ya kumalizika vita vya bushiri vilivyokuwa vikipinga biashara ya utumwa pamoja na kazi ngumu walizokuwa wanatumikishwa waafrika dhidi ya wajerumani walionunua eneo la ukanda wa pwani wa Afrika ya mashariki kutoka kwa sultani.
Wajerumani katika kupanua eneo la himaya yao ndani  zaidi na hasahasa katika maeneo ya milima ya usambara yenye kuwa na ardhi nzuri pamoja na hali ya hewa ya ubaridi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na biashara ilipelekea 


kujengwa kwa barabara ya reli kutoka Tanga mpaka Moshi pamoja na miundo mbinu ya mitandao ya njia za barabara zilizoendelezwa na hii ilihusisha barabara ya kutokea mombo  kuelekea maeneo ya milimani na kupelekea kupatikana kwa kituo kilichofahamika kama (WILHELMSTHAL)kikifahamika leo hii kama wilaya ya LUSHOTO.
LUGHA YA KISWAHILI
Lugha ya Kiswahili ilifanywa rasmi kuwa lugha maalumu ya watawala wajerumani na vijana wa kiafrika wa kipindi hicho wakaanza kupatiwa elimu katika shule ambayo mpaka leo hii bado ipoikifahamika kama Tanga school iliyokuwa maalumu kwa ajili ya wafanyakazi waafrika wa ngazi ya chini katika utawala wa wajerumani. 



Mji wa Tanga wa leo hii katika kipindi cha wakati wa utawala wa wajerumani uliendelezwa katika maeneo tofauti tofauti ya makazi ya wananchi,biashara na majengo ya serikali.
Mwishoni wa karne ya 19 hivi, mji wa Tanga tayari ilifikia idadi ya watu zaidi ya 5000.Mji wa Tanga kihistoria ilikuwa ni sehemu ya kituo muhimu sana katika biashara na makazi kwa pamoja na miji mingineyo kama vile
Dares-salaam, ujiji,Tabora,Bagamoyo,Pangani na kilwa kivinje


Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba kihistoria miji ya ujiji,Tabora,Bagamoyo,Pangani,pamoja na kilwa kivinje ni miji ambayo ilitumika aidha kama sehemu za njia za msafara wa biashara ya watumwa na bandari za nchi kavu katika kuwasafirisha watumwa kwenda sehemu nyinginezo kama vile Zanzibari na bara Arabuni.Ilipofikia mwaka 1913 tayari mji wa Tanga ulikuwa ni moja ya miji mikubwa kabisa katika miji 4 nchini Tanzania.  


Wakati wa kipindi cha uhuru wa mwaka 1961 Tanga ilikuwa mji wa pili
kwa ukubwa baada ya Dares-salaam.
Wakati wote wa kipindi cha wakati wa kihistoria ya kikoloni vyanzo vikuu vya kiuchumi vya mkoa wa Tanga ilikuwa ni pamoja na zao la kibiashara la mkonge ambalo lililetwa Tanga kutokea mji wa Florida katika nchi ya Marekani katika miaka ya 1893 na hatimaye kuweza kuufanya mkoa wa Tanga kuwa maarufu katika uzalishaji wa zao la mkonge (katani) 


na usafirishaji kitaifa na kimataifa. Ilipofikia mnamo mwaka 1914 wa mwezi Novemba mji wa Tanga uliweka historia ya kijeshi kupitia msaada wa kituo kipya cha meli- kanali wa kijerumani aliyojulikana kama Von –lettow Vorbeck akiwa na kikosi chake cha askari waafrika pamoja na walowezi wa kijerumani walipigana vilivyo katika kuulinda mji wa Tanga dhidi ya meli za kivita za waingereza .  

Katika vita hivi wajerumani wakishirikiana na askari waafrika walishinda vita hivyo pamoja na ukweli wa mambo ya kwamba idadi ya majeshi ya waingereza ilikuwa kubwa dhidi ya wajerumani na wafuasi wao.

WAKAZI WANANCHI WENYEJI WA MKOA WA TANGA 
Ni pamoja na makabila ya wasambaa,Wabondei,Wadigo na Wazigua.Lakini vilevile kuna makabila mengineyo madogo madogo.


SHAABANI BIN ROBERT
Mwandishi maarufu na hadhina na urithi ya mkoa wa Tanga na Taifa katika kuikuza  lugha ya Kiswahili

HISTORIA YAKE SHAABANI BIN ROBERT
Shaabani bin Robert alizaliwa mwaka 1909 katika wazazi wa kabila la wayao linalopatikana kijiografia katika maeneo ya mikoa ya kusini nchini Tanzania.Kijiji cha machui kinachopatikana kijiografia kusini mwa mji wa Tanga takribani kilomita zaidi ya 10 hivi ndipo sehemu alipozaliwa shaabani bin Robert moja ya waandishi wakubwa na maarufu katika kuikuza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania na barani Afrika ambaye Tanzania imeweza kutoa.
ELIMU YAKE SHAABANI BIN ROBERT 
Shaabani bin Robert alipata elimu yake katika shule ya msimbazi mkoani
Dares-salaam na alianza kazi wakati wa kipindi cha utawala wa wakoloni waingereza kama mtumishi karani katika kitengo cha ushuru katika mji wa pangani mnamo mwaka 1926.Wakati wa kipindi cha uhai wa maisha yake alitoa kazi nyingi za kiuandishi.
Kuanzia mwaka 1944 mpaka 1946 alijiunga na kitengo cha idara ya wanyama pori ikifuatiwa baadaye na kazi katika idara ya mipango katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tanga mjini mpaka mnamo mwaka 1952
MAISHA YA KIFAMILIA  YA SHAABANI BIN ROBERT
Shaabani bin Robert alioa mara mbili na kubahatika kuwa na watoto 10.Alifariki bado akiwa ma umri wa rika la ujana mnamo mwaka 1952 na kuzikwa katika kijiji alichozaliwa cha Machui ambapo kaburi lake bado lipo mpaka leo hii.Mungu ailaze roho ya marehemu peponi.Amina.
JIOGRAFIA YA MKOA WA TANGA
Mkoa wa Tanga kijiografia unapatikana upande wakaskazini mashariki mwa Tanzania na inapakana kimipaka na mikoa ya Kilimanjaro na Dares-salaamkatika upande wa kusini pamoja na nchi jirani ya Kenyakatika upande wa kaskazini.Mkoa wa  Tanga una sehemu kuu 4 zenye kuwa na fursa za shughuli za kiutalii.Manispaa ya mji wa Tanga inapatikana kijiografia katika mwambao wa bahari kuu ya hindi wakati ambapo shughuli zote za kiuchumi hufanyika  katika maeneo mengineyo.
Manispaa ya mji wa Tanga ina utajiri  mkubwa katika historia, utamaduni,vivutio vya kiutalii pamoja na viumbe hai mbalimbali vinavyopatikana katika mazingira ya makazi ya maji baharini.Kusini mwa mji wa Tanga kijiografia kunapatikana mji wa kibiashara wa pangani ambao unafahamika zaidi toka karne ya 19.Mji wa pangani una fursa za utajiri wa maliasili za fukwe na moja ya sehemu nzuri  na bora katika matembezi ya kitalii ya ufukweni.Kusini zaidi ya mji wa Tanga panapatikana hifadhi ya taifa ya Saadani yenye kuwa na utajiri wa mali asili za fukwe pamoja  na wanyamapori wanaofurahia upepo mzuri mwanana wa baharini.Upande wa magharibi wa mji wa Tanga  na milima ya mashariki ya usambara panapatikana kituo chenye manzari nzuri yenye kupendeza cha gari moshi cha msitu wa Amani maarufu kwa uhifadhi wa viumbe hai adimu mimea na wanyamapori.
Katika mkoa wa Tanga kwa ujumla panapatikana maeneo mengi yenye kuwa na fursa za shughuli za kiutalii pamoja na majengo ya kale yenye kuwa na utajiri wa kihistoria na utamaduni.Fukwe zenye kuwa na uoto wa asili wa mimea ya miti ya mikoko pamoja na safu ya milima ya usambara mashariki na magharibi.Mapango ya Amboni,visiwa vya Torten,Yambe,Rulenge,Nyamaku na mwarongo.Magofu ya kale ya Tongoni,kijiji cha ndumi,makumbusho ya Tanga,vilima vya ndola,majengo ya kale ya wajerumani pamoja na msitu wa asili wa Amani.   
Katika wilaya ya Muheza panapatikana mnara wenye kuwa na kumbukumbu ya muasisi wa uskauti duniani na kundi la kwanza kabisa laUskauti lililofahamika kamamsalabani .Mnara huu wa kumbukumbu ulijengwa na serikali mwaka 1994 katika kuadhimisha miaka 75 ya shughuli za Uskauti nchini Tanzania.
Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba mnara huu uliwekwa  katika wilaya ya Muheza, kwasababu Lord Robert Stephenson Smyth-Baden Powell (mwaka 1857mpaka 1941)alikuwa ndiye Luteni jenerali wa jeshi la kiingereza aliye kuwa maarufu na muasisi wa jeshi la uskauti katika mwaka 1907 ambaye alitembea kijiji chamagilla.
WILAYA ZA MKOA WA TANGA
Mkoa wa Tanga umegawanyishwa katika wilaya 8 na kila wilaya zinajitegemea kimamlaka na uongozi katika utendaji wa kazi za ujenzi wa taifa  Tanzania.Wilaya hizini kama zifuatavyo;
WILAYA YA LUSHOTO
Wilaya ya lushoto ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4000 na jumla ya wakazi wananchi wanaofikia zaidi ya 400.
WILAYA YA KOROGWE
Wilaya ya korogwe ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 3100,na jumla ya wakazi wananchi takribani zaidi ya 200.
WILAYA YA HANDENI
Wilaya ya handeni ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8000 na jumla ya wakazi wananchi zaidi ya 248.
WILAYA YA TANGA MJINI (MANISPAA)
Wilaya ya Tanga mjini (manispaa)ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa         kilomita  za mraba 600 na jumla ya wakazi wananchi zaidi ya 244.
WILAYA YA MUHEZA
Wilaya ya muheza ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2300 na jumla ya wakazi wananchi zaidi ya 171.
WILAYA YA KILINDI
Wilaya ya kilindi ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5500 na jumla ya wakazi wananchi zaidi ya 144.
WILAYA YA MKINGA 
Wilaya ya mkinga ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 3000 na jumla ya wakazi wananchi zaidi ya 106.
WILAYA YA PANGANI 
Wilaya ya pangani ina ukubwa wa eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,700 na jukla ya wakazi wananchi zaidi ya 50.
HALI YA HEWA YA MKOA WA TANGA
Mkoa wa Tanga kijiografia unapatikana katikamwambao wa pwani ya Afrika ya mashariki na hali yake ya hewa kawaida ni ya joto ambapo kwa wastani ni nyuzi joto 28.
Upepo mwanana uvumao toka baharini huifanya hali ya hewa ya mkoa wa Tanga kuwa yenye mandhari nzuri yenye kupendeza karibia mwaka mzima wakati ambapo maeneo ya miinuko katika wilaya za korogwe na Handeni kawaida huwa na joto wakati wa kipindi cha mchana na wakati wa usiku hali ya hewa ya ubaridi huwepo.
Katika maeneo ya mazingira ya makazi ya milimani baina ya maeneo ya ukanda wa pwani pamoja na maeneo ya milimani kaskazini kawaida hali ya  hewa ya joto hupungua zaidi wakati wa usiku chini ya nyuzi joto 10 hivi –katika kipindi cha miezi ya baridi cha mwezi Juni na Julai.Kipindi cha wakati wa miezi ya kipindi cha joto kawaida huwa mwezi oktoba mpaka Februari.Kipindi kikuu cha wakati wa msimu wa mvua za masika kawaida huanzia mwezi Aprili mpaka mwezi Mei mwishoni wakati ambapo hutokea mvua kunyesha wakati wa usiku na mchana jua likiwaka.
VIVUTIO VIKUU VYA UTALII MKOANI TANGA 
MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MJINI -TANGA
Jengo jipya la boma ni sehemu ambayo jengo la utawala wa kipindi cha utawala wa kijerumani likitumika hivi karibuni kama makumbusho.
                  
KISIWA CHA YAMBE
Kisiwa cha yambe kijiografia kinapatikana kusini mashariki mwa ghuba ya Tanga mkabala karibu na Rasi ya nyamakuu peninsula.Kisiwa hiki cha yambe kimezungukwa na matumbawe na kimefunikwa kabisa na uoto wa asili wa mimea ya miti ya misitu ya mikoko.
MAGOFU YA KALE YA KIJIJI CHA NDUMI
Magofu ya kale ya kijiji cha ndumi kijiografia kinapatikana karibu kabisa jirani na Rasi ya nyamakuu peninsula ambapo hakuna watu wakiishi katika maeneo hayo.Kihistoria inasemekana ya kwamba magofu ya kale ya kijiji cha ndumi yalikuwepo tangu karne ya 14.
KISIWA CHA RULENGE
Kisiwa cha Rulenge kijiografia kinapatikana kikipakana * kimipaka*na ghuba  za Tanga pamoja na kwale katika upande wa kaskazini ya mji wa Tanga.
KISIWA CHA TORTEN
Kisiwa cha Torten kijiografia kinapatikana katika ghuba ya Tanga moja kwa moja mkabala na Bandari ya Tanga.Kisiwa  hiki cha Torten kimezungukwa na kufunikwa na uoto wa asili wa mimea ya miti ya misitu sambamba kabisa na miti mikubwa ya mibuyu lakini panapatikana magofu ya kale ya makazi ya watu walioishi hapo zamani.Wakati wa kipindi cha zama za utawala  wa Kireno katika eneo hilo lilitumika kama eneo la magereza kwa ajili ya kuhifadhi wafungwa.
MAJI MOTO YA GALLANOS
Takribani umbali wa mwendo wa kilomita 8 kutoka manispaa ya mji wa Tanga na vilevile kilomita 3 hivi kutoka katika mapango ya Amboni panapatikana eneo la maji moto ya Gallanos.

MAPANGO YA AMBONI
Mapango ya asili ya Amboni kijiografia yanapatikana umbali wa mwendo wa takribani kilomita 8 hivi kutoka kaskazini mwa mji wa Tanga.
MAGOFU YA KALE YA TONGONI
Magofu ya kale ya Tongoni yako chini ya usimamizi na uendeshaji wa idara ya mambo ya kale ya wizara ya mali asili na utalii.Tongoni ni kijiji kidogo  chenye shughuli za kiuchumi za uvuvi wa samaki na kinapatikana umbali wa kilomita  17 kusini mwa mji wa Tanga.



Magofu  ya kale ya Tongoni  ni pamoja na misikiti,makaburi,masalia ya majengo ya makazi ya kale ya waarabu wa mwanzo katika uajemi
MNARA WA KUMBUKUMBU  YA USKAUTI  MUHEZA
Mnara huu wa kumbukumbu ulijengwa na serikali mwaka 1994 katika kuadhimisha miaka 75 ya shughuli za uskauti nchini Tanzania.Lord Robert Stephenson Smyth Baden Powell (katika miaka ya 1857 mpaka 1941) ambaye ndiye muasisi wa uskauti duniani alitembelea kijiji cha magilla katika mwaka 1907.






No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!