Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.
Kuna aina kuu mbili za kisukari:
- Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.
- Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.
Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa. Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).
Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanyamazoezi au sababu za kurithi (genetics). Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari. Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).
Baadhi ya dalili kuu za kisukari ni:
- kiu iliyozidi
- kukojoa mara kwa mara
- kupatwa na ganzi kwenye miguu na mikono
- kujisikia mchovu
- kutoona vizuri
- kuongezeka njaa
- kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Ikiwa daktari atakuona una dalili za kuwa na kisukari, ata kutaka ufanye jaribio la kuiandaa glukozi katika usawa wake wa chini kabisa kwenye damu (fasting plasma glucose test – fpgt), kwa sababu hiyo, atakutaka ubaki bila kula kitu chochote kwa muda usiopungua masaa nane kabla ya kukupima, ambapo kwa kawaida huwa ni asubuhi ili kupata uwezekano wa damu sukari kuwa katika usawa wake wa chini kabisa.
Kisha atachukua damu toka kwenye mkono na kuipima na kulinganisha matokeo na uwiano ufuatao:
- Chini ya 99 mg/dl ni kawaida
- 100 – 125 mg/dl ni hatua za mwanzo za kisukari
- Zaidi ya 126 mg/dl ni kisukari.
Kisukari ambacho hakikudhibitiwa kinaweza kusababisha mwili kulazimika kuanza kuchoma mafuta ili kuzarisha nishati (diabetic ketoacidosis), hii kwa kawaida hutokea kwa watu wenye kisukari cha aina ya kwanza ambapo glukozi inaweza kuingia kwenye seli bila insulini.
Kitendo cha mafuta kutumika kuzarisha nishati huzarisha taka nyingi zaasidi zilijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘Ketones’.
Taka hizi (Diabetic ketoacidosis – DKA) hujijenga kwenye mzunguko wa damu na kusababisha pumzi fupi, mauzauza na kutapika na mwishowe kukuwekea koma na hata kusababisha kifo.
DKA haijitokezi sana siku hizi ahsante kwa insulini na vifaa rahisi kutumia kufuatilia damu sukari.
Wakati damu sukari inapokuwa nyingi na damu inapokuwa imetulia, nene na hafifu (hyperosmolar syndrome), husababisha kukojoa mara nyingi ili kuilazimisha sukari iliyozidi kutoka nje. Ikitokea hivyo, utapatwa na upungufu mkubwa wa maji na unaweza kushikwa na mikakamao ya miguu, mapigo ya moyo kwenda mbio, mauzauza, msukosuko, au hata kuelekea kwenye koma. Hii huwatokea watu wenye kisukari aina ya pili ambao hawafuatilii kujuwa kiasi cha damu sukari yao mwilini.
Moja kati ya matatizo makubwa ya kisukari ni kitendo cha kushuka kwa kiasi kikubwa cha damu sukari mwilini (hypoglycemia), hii hutokea wakati damu sukari inazarishwa kidogo kutokana na kutumia kiasi kingi cha insulini au kukaa muda mrefu bila kula chochote na huku ukiwa umetumia insulini au ulinusa harufu ya chakula fulani.
Zifuatazo ni dalili za kushuka kwa damu sukari mwilini:
- Kichwa kuuma
- Mauzauza
- Mapigo ya moyo kwenda mbio
- Kutokwa na jasho jingi
- Kuona vitu viwili katika kimoja.
Ikiwa damu sukari itashuka kufikia usawa wa 50 – 70 mg/dl, unaweza kujisikia kuwa na hali zifuatazo:
- Kuishiwa nguvu
- Kusinzia na kizunguzungu
- Kuona nukta nukta kabla ya macho yako
- Mwili unaweza kuwa kama uliopooza.
Wakati damu sukari imeshuka kufikia 30 – 45 mg/dl, unaweza kwenda kwenye koma (deep sleep) na kufa ikiwa hautapewa sukari ya haraka kama inayopatikana kwenye juisi ya chungwa (huitwa muokoaji kwenye uwanja wa madawa), sukari halisi au peremende ya sukari ili kupandisha kiwango cha damu sukari mwilini
Namna moja ambayo kisukari kinaweza kujipenyeza taratibu kwenye miili ya watu, ni pale insulini inapofanya ukaidi bila wao kujua, ukaidi huu wa insulini ukitokea, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupatwa na kisukari wakati fulani katika safari yako ya kuishi.
Ukaidi wa insulini (insulin resistance) ni wakati ambapo mwili unazarisha insulini lakini hauitumii ipasavyo.
Insulini ni homoni inayotengenezwa na kongosho ili kuusaidia mwili kuitumia glukozi kwa ajili ya kuzarisha nishati. Glukozi ni aina ya sukari ambayo ni chanzo kikuu cha nishati ya mwili.
Mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, hukimeng’enya chakula na kuwa glukozi ambayo kisha husafiri kwenye mkondo wa damu mwili mzima. Glukozi inapokuwa kwenye damu huitwa damu glukozi, pia hujulikana kama damu sukari. Wakati damu sukari inapopanda juu baada ya kula, kongosho huitoa insulini ili kuziwezesha seli za mwili wako kuitumia glukozi.
Mtu anapokuwa katika hali ya ukaidi wa insulini, mishipa, mafuta na Ini lake vinakuwa haviitiki vema kwa insulini, kwa sababu hii, mwili wake utaihitaji insulini zaidi ili kuiwezesha glukozi kuziingia seli.
Kongosho litajaribu kukidhi ongezeko la uhitaji huo wa insulini kwa kuizarisha insulini nyingi zaidi. Hatimaye kongosho halitaweza kuendelea kumudu kuzarisha kiasi hicho kingi cha insulini. Insulini na Glukozi iliyozidi, vitajijenga ndani ya mkondo wa damu vikiandaa ngazi kuelekea kisukari.
Katika kitabu cha dr.Batman, ‘your bodies many cries for water’ anasema ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.
Ubongo pia utapandisha juu kiwango cha sukari kwenye damu ili kuuwezesha kufanya kazi zake vizuri. Cha kushangaza ni kuwa, mwili unaihitaji insulini ili kuuwezesha kuitumia sukari kama chanzo cha nishati, lakini kamwe ubongo hauihitaji insulini ili kuupelekea mahitaji yake ya nishati.
Katika kisukari, ubongo unajipa moyo wenyewe kama vile daktari ampavyo moyo muathirika wa kisukari kwa kutumia dripu zenye sukari na chumvi (intravenous fluid treatment).
Watu wengi wenye kisukari huwa hawaelewi ni kwanini wanakuwa na damu sukari nyingi wakati waamkapo asubuhi ikiwa hawakula kitu chochote kabla ya kwenda kulala. Sababu ni kuwa, usiku unapokuwa umelala, mwili hufanya kazi kwa bidii kujiripea wenyewe, katika kufanya hivyo, mwili hutumia sukari. kwakuwa haukula chochote kabla ya kwenda kulala, mwili lazima ujile wenyewe (cannibalize off itself) ili kuliwezesha Ini kutengeneza sukari kwa ajili ya nishati.
Ubongo, ambao ni kituo kikuu cha udhibiti wa kazi zote za mwili, utagunduwa kuwa hakuna kiasi cha kutosha cha sukari kwenye damu kwa ajili ya matumizi yake, na kwa sababu hiyo utaliamuru ini kutoa mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari ikiwa damu itaihitaji. Hii ndiyo sababu ya kupanda kwa kiwango cha sukari asubuhi kama hukula chochote kabla ya kwenda kulala.
Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi. Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan’ ili kuubeba mwili usiku mzima.
Katika kuepuka sukari, baadhi ya watu wenye kisukari huamua kutumia viongeza sukari visivyo vya asili (artificial sweeteners). Viongeza utamu hivi visivyo vya asili pia huongezwa katika soda na juisi nyingi za viwandani. Unapoweka sukari ya kutengenezwa ulimini au unapokunywa kinywaji au kula chakula kilichoongezwa sukari za kutengenezwa, ulimi utauambia ubongo kuwa sukari inakaribia kuja, ubongo utaliambia Ini liache kuendelea kutengeneza sukari bali liihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye na lijiandae kuishughurikia sukari iliyopo njiani kuja. Muda wote ini huwa bize likitengeneza sukari mwilini.
Ubongo upo makini sana (very smart), baada ya muda yaani baada ya hiyo sukari ya kutengenezwa kutua chini tumboni utagundua kuwa hakuna sukari iliyoliwa bali ulilaghaiwa au ulidanganywa. Dakika hii mzunguko wa damu unakuwa katika udharura wa uhitaji wa sukari.
Fikiri: Kila siku unaenda dukani kununua unga wa ugali kilo moja. Siku moja unafika dukani mwenye duka anakuambia unga umebaki kilo tatu na hajuwi lini atapata mzigo mwingine. Utafanya nini?. Utafanya kila uwezalo uzichukuwe hizo kilo tatu zilizopo kama tahadhari kesho usishinde bila kula.
Ndicho kinachotokea mwilini. Ubongo ukishagunduwa kuwa iliyoliwa haikuwa sukari na ulishaliamuru Ini kupumzika kuitengeneza sukari kwenye mzunguko, utaliamuru Ini kuipatia damu mara mbili mpaka tatu ya kiasi cha sukari zaidi ya inavyohitajika!. Sasa unapoenda kupima kiasi cha damu sukari, unajikuta huelewi nini cha kufanya kwa sababu kipo juu mno. Na sasa lazima uchomwe insulini ili kuishusha damu sukari.
Dr.Batman, anasema; ‘kwa sehemu kubwa, kisukari ni matokeo ya kukosa maji, chumvi, magnesiamu, asidi amino (tryptophan) ipatikanayo kwenye mayai, maharage, vyakula jamii ya karanga na jibini, vitamini B6, zinki na mazoezi’.
Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha) na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali’ ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.
VITU MHIMU VYA KUZINGATIA KWA MTU YEYOTE ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI:
- Acha kabisa soda ya aina yeyote pamoja na juisi za viwandani hadi hapo utakapopona
- Acha chai ya rangi na kahawa
- Jishughulishe zaidi na mazoezi
- Ongeza unywaji maji na utumiaji wa chumvi hasa ya mawe ile ya baharini
- Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito ule unaotakiwa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
- Tumia vyakula ambavyo havijakobolewa, mfano kama ni ugali tumiaunga wa dona na siyo wa sembe n.k
No comments:
Post a Comment