Wednesday, 9 December 2015

BAYPORT YAMUUNGA MKONO DR MAGUFULI KWA VITENDO, YAPAKA RANGI NA USAFI KATIKA SHULE YA MSINGI HEKIMA


Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akipaka rangi katika ukuta wa shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.




Meneja wa Oparasheni wa Bayport Financial Serviices, Charles Mgeta, akizungumza na waandishi wa habari juu ya taasisi yao kuamua kufanya usafi, kutunza mazingira na kuipaka rangi shule ya msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, Wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto mwenye kofia na miwani akishiriki kufanya usafi katika shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, asubuhi.

Wafanyakazi wa Bayport, walimu na wanafunzi wakijiandaa kufanya usafi mbele ya jengo la shule ya Hekima, kabla ya kuanza kupakwa rangi.

Mchambuzi wa Miradi wa Bayport Financial Services, Joseph Munga, kulia akishiriki kupaka rangi katika shule hiyo ya msingi Hekima.



TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na utoaji wa mikopo, jana imemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi, kutunza mazingira na kupaka rangi shule ya Msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku wakianza kwanza kusafisha eneo la Makao Makuu ya ofisi yao, kabla ya kuelekea hapo. Tukio hilo liliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bayport, John Mbaga, pamoja na zaidi ya wafanyakazi 80 kwenye taasisi hiyo inayotoa mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, bila kusahau wajasiriamali katika mradi wao wa mikopo ya viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Shughuli hiyo Ilianza mishale ya saa tatu asubuhi ambapo Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wa Bayport walianza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo, pamoja na upakaji wa rangi katika baadhi ya madarasa katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi 1900, ukiacha idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza watakaonza shule mapema mwakani.
Wafanyakazi wa Bayport Financial Services wakiendelea na usafi katika shule ya msingi Hekima.


Akizungumza katika tukio hilo leo asubuhi, Mkurugenzi wa Bayport Financial Servivces, John Mbaga, alisema kwamba wameamua kuchagua shule ya Tandale kwa sababu inahitaji kuungwa mkono kutokana na eneo iliyopo pamoja na changamoto mbalimbali za kimaisha. Alisema baada ya rais kuagiza kwamba Sikukuu ya Uhuru 9 Desemba iendane na kazi ya kufanya usafi na utunzaji wa mazingira, Bayport iliamua kwenda mbali zaidi kwa kuhakikisha kwamba wanaipaka rangi shule hiyo ili ionekane safi, tofauti na ilivyokuwa awali.
Usafi ukiendelea shuleni hapo
Usafi ukiendelea
“Tunamuunga mkono Dr Magufuli na serikali yake kwa vitendo, hivyo si usafi tu, ila tumeirudisha shule ya Msingi Hekima kwenye upya wake, huku tukiamini kuwa tutaendelea kujikita zaidi katika mambo ya kijamii, hususan katika suala zima la elimu kwa kusaidia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wetu” alisema Mbaga.

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamefurahia kushirikiana na walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Hekima kufanya nao usafi na kutunza mazingira ya eneo la shule hiyo inayotumiwa na watoto wengi kutoka kwenye Kata hiyo ya Tandale. “Bayport ni taasisi ya Watanzania wote, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, hivyo naamini itaendelea kutoa huduma bora zenye kuwakwamua wateja wetu,” alisema Cheyo.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Hekima, Hussein Mohamed, aliishukuru Bayport kwa kujitolea kurudisha upya wa shule yao kwa kuamua kuipaka rangi, pamoja na kushirikiana nao katika 9 Desemba kufanya usafi, jambo ambalo ni muhimu ili kujiepusha na magonjwa ya miripuko, ukiwamo ugonjwa wa Kipindupindu.

“Hatuna cha kuwalipa Bayport kwa kujitolea kwao kwetu, hivyo tunawaombea kwa Mungu, ingawa tunazidi kuwaomba waendelee kuwa karibu na sisi kwa kutusaidia mambo mbalimbali ili tufanikishe kwa vitendo kuwapatia watoto wetu elimu bora ili kuwaandalia maisha bora wanafunzi hawa ambao licha ya changamoto kadhaa zinazotukabili, ila ufaulu wao umekuwa ni mkubwa, jambo linalotutia moyo,” alisema Mohamed. Bayport ni moja ya taasisi zinazofanya juhudi kubwa kuwakwamua wateja wao, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi kwa kupewa mikopo isiyokuwa na amana wala dhamana, huku huduma hizo zikipatikana kwa urahisi kutokana na kuenea kwa matawi zaidi ya 80 katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.







No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!