Tuesday, 17 November 2015

WATUMIAJI INSTAGRAM WASAIDIA WAGONJWA OCEAN ROAD


Mmiliki wa Twaiba Classic Centre akitoa michango kwa baadhi ya wagonjwa.
Wana-Instagram wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Hospitali ya Ocean Road.

KIKUNDI cha watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram jijini Dar wanaounda umoja wa kusaidia wagonjwa katika hospitali kubwa jijini, wametoa msaada kwa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road ikiwa ni moja ya taratibu walizojipangia.
Wana-Instagram hao wanaoongozwa na mmiliki wa duka la Twaiba Classic Centre na akaunti ya Instagram yenye jina hilohilo walitoa msaada huo wikiendi iliyopita baada ya kukusanya michango kwa wiki nzima kwa kupitia namba walizoziweka kwenye mitandao yao ya kijamii.
Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kutoa msaada huo, mmiliki huyo wa Twaiba Classic Centre alisema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akitaka kuwasaidia wagonjwa wanaouguza magonjwa hospitali mbalimbali jijini hapa bila kuwa na msaada wowote wa kifedha au kugharamia matibabu ambapo aliamua kubuni njia hiyo na kusema kuwa amelazimika kutangaza misaada hiyo ili watu waongezeke kujitolea kuwasaidia wagonjwa kupitia vikundi mbalimbali.
“Mwanzoni kuna watu walidhani nafanya utani lakini kweli tumekuwa tukipokea misaada hadi kutoka nchi za nje na watu wameguswa na hali za wagonjwa hawa ndiyo maana wamejitolea. Tunaomba waendelee kuwa na sisi kwa kuwa kila mara tunatembelea hospitali mbalimbali kuwasaidia chochote,” alisema mmiliki huyo na kuongeza kuwa mtu yeyote atakayeguswa n hali hiyo atoe michango yake kupitia namba 0654 184747 na 0758 180355.
(Picha/ Chande Abdallah/ GPL)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!