Saturday 7 November 2015

WAANDISHI WA HABARI WALIOSHINDA UONGOZI KISIASA WATAKIWA KUACHA KAZI

Image result for PRESS

MUUNGANO wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC), umewataka waandishi wa habari walioshinda nafasi za uongozi wa kisiasa ukiwemo ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni, wajitokeze hadharani kuutangazia umma kuwa sasa wanaachana na kazi za uandishi wa habari.


Kauli hio ilitolewa jana na Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano mkuu wa UTPC na Rais wake, Kenneth Simbaya.
Mkutano huo wa siku mbili , umehusisha pia na uchaguzi mkuu wa viongozi wa UTPC na wajumbe wa Bodi ambao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo , na ulikuwa na kaulimbinu ya ‘ Tumia Klabu za Waandishi wa Habari kwa maendeleo ya mkoa wako’.
Hivyo alisema kuwa, sheria za klabu za waandishi wa habari zilizopo chini ya UTPC hairuhusiwi kwa mwandishi wa habari kuwa ni kiongozi wa vyama vya siasa, licha ya kila mmoja kuwa na uhuru wa kushiriki masuala ya siasa .
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa UTPC, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, baadhi ya waandishi wa habari walishiriki kufanya kampeni za siasa kwa wagombea na vyama vya siasa.
“Tangu mwanzo tulifanya makosa kwa suala hili halikuwekwa wazi kwa mwandishi wa habari ama chombo cha habari kijiweke wazi ...mwandishi wa habari hakatazwi kuingia kwenye siasa isipokuwa akifanya hivyo ni budi ajiondoe kwenye uandishi wa habari, “ alisema na kuongeza. “
Anatakiwa ajitokeze hadharani na kutangaza kuwa anajiuzulu kazi hiyo , na hata chombo chenye mrengo wa kisiasa wa chama fulani kinapaswa kuujulisha umma kuwa kinamuunga mkono mgombea fulani,” alisisitiza. “
Lakini mambo haya yamefanyika kisirisiri na tunashuhudia waandishi wa habari sasa wameanza kusutana wao kwa wao kwa kuitana ‘Ukawa’ na ‘UCCM’” alisema Karsan.
Hivyo aliwataka waandishi wa habari kurudi mwenye mstari wa kuandika habari za kuwaunganisha wananchi katika masuala ya ujenzi wa taifa lao badala ya kuendelea kuandika habari za kikampeni, kwani uchaguzi mkuu umemalizika na mshindi amepatikana.
Naye Simbaya, aliwataka wanachama na viongozi watakaochaguliwa kuiongoza UTPC ijayo watumie uelezi wao kwa kushirikiana kuifikisha mbali zaidi kimaendeleo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!