Thursday, 26 November 2015
Uongozi wa Bunge umesema kuwa mkopo wa gari kwa wabunge utabakia kuwa milioni tisini(90).
Msemaji wa Bunge amesema kuwa hawajapata malalamiko rasmi kutoka kwa wabunge kuwa wanahitaji kuongezea fedha hizo zifikie milioni 130 kutokana na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani.
Mbunge Ezekiel Maige amesema kuwa afadhali Serikali iwanunulie magari kabisa kuliko kuwapa fedha.
Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Abdallah Mtolea amesema wapewe fedha wakanunue wenyewe, pia amedai kuwa bei ya gari Land Cruiser(Mkonge) ambayo wabunge wanatakiwa kununua gharama yake sokoni ni milioni 130.
Awali baadhi ya wabunge walidai kuwa wapewe milioni 130 kutokana na kupanda kwa bei ya magari wanayotakiwa kununua.
Wabunge wa Bunge la 10 walipewa milioni 90 za kununua gari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment