Friday 6 November 2015

MBARONI KWA KUWAFUNGIA WATOTO YATIMA NA KUWAWEKA KINYUMBA

MKAZI mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Bagule (61) mkazi wa Kilimahewa Kata ya Maili moja Mjini Kibaha Mkoani Pwani, anatuhumiwa kuwafungia watoto yatima ndani na kuwaweka kinyumba.


Taarifa zilizoifikia FikraPevu na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani humo zinaeleza kuwa, Joseph (61) anatuhumiwa kuwafungia wajukuu zake wawili akiwemo mwenye umri wa miaka (16) na Mtoto wa Dada yake mwenye miaka (25) ambapo amezaa nao watoto.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jafari Ibrahim, ameithibitishia FikraPevu kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Aidha, amesema mbali na kumshikilia mtuhumiwa, kwasasa wanafanya vipimo vya vinasaba (DNA) kwa ajili ya kupata uhakika kama ni kweli mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuzaa na wajukuu wake kuwa ni kweli au la!
FikraPevu inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu na kadri itakavyopata taarifa zaidi itawajulisha wasomaji wake kile litakachojiri.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!