Monday 9 November 2015

KIJO KISIMBA ANUSURIKA KIFO


MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akitembelea kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.


Gari hiyo yenye namba za usajili T336 CTT aina ya Toyota LandCruiser GX V8, lilipinduka jana asubuhi, baada ya kuacha njia katika Narabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam.
Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva wa mkurugenzi huyo, lilipinduka kwenye eneo maarufu la taa za Aga Khan likiwa na abiria watatu, akiwemo Bisimba.
Akizungumza katika mahojiano na Radio One jana, Mkurugenzi Msaidizi wa LHRC, Imelda Urio alisema Bisimba amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan wakati abiria wengine waliruhusiwa baada ya matibabu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!