Monday, 12 October 2015

ZIARA YA RAIS HAGEB GEINGOB NA MKEWE NCHINI TANZANIA.

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob mara baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kiserikali nchini Tanzania tarehe 11.10.2015.


2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na mgeni wake Mke wa Rais wa Namibia Madam Monica Geingos wakiwapungia mikono wananchi waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Madam Monica ameambatana na mumewe Rais Hage Geingob kwa ziara ya kiserikali nchini.
3
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma wakiwakaribisha wageni wao Rais Hage Geingob na  Mkewe Madam Monica Geingos Ikulu. Kiongozi huyo wa Namibia aliwasili nchini tarehe 11.10.2015 kwa ziara ya kiserikali.
4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo ya faragha-tete a tete-na mgeni wake Mke wa Rais wa Namibia Madam monica Geingos huko Ikulu tarehe 11.10.2015.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akigonganisha glasi na Rais Hage Geingob wa Namibia wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Kikwete huko Ikulu tarehe 11.10.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!