Thursday, 1 October 2015

UMASIKINI WAKOSESHA VIJANA MILIONI MOJA MASOMO YA JUU


Serikali imesema wanafunzi milioni moja wanaomaliza shule za msingi na sekondari kila mwaka nchini wamekuwa wakikosa fursa ya kuendelea na masomo ya juu kutokana na wengi wao kutoka katika familia maskini.

Hayo yalisemwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘Kuwawezesha Vijana Kiuchumi’, katika Chuo cha Ufundi (Veta), Kipawa, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema ongezeko hilo la wanafunzi wanaokosa fursa ya kuendelea na elimu ni  changamoto kubwa kwa serikali ambayo inatafuta namna ya kuongeza nafasi za mafunzo katika vyuo vya ufundi stadi ili kukidhi mahitaji kulingana na wimbi hilo.
Dk. Bilal alisema serikali imeanza kutekeleza mpango wa kukuza na kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi, ambapo chini ya mpango huo hatua za awali za kuimarisha elimu na stadi  mbalimbali za ufundi pamoja na kusitisha utaratibu wa kubadili vyuo vya ufundi kuwa vyuo vikuu zimechukuliwa. 
“Serikali imefanya hivyo kwa kutambua kuwa yapo mahitaji makubwa katika soko la ajira kwa wataalam wanaohitimu kutoka vyuo hivyo vya ufundi,” alisema. 
 Dk. Bilal alisema mradi huo umekuja kwa wakati muafaka kwani unatekeleza malengo ya serikali, hivyo utumike ipasavyo kwa kutoa fursa za mafunzo bora ya ufundi stadi yatakayowawezesha vijana kupambana na umaskini.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Plan International Tanzania,  Gerald Maghash, alielezea kuwa mradi huo wa miaka mitatu utawanufaisha vijana wanaotoka katika familia maskini 9,100, katika wilaya tisa zilizoko katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Kisarawe,   Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.
“Kati ya vijana hao asilimia 53 ni wasichana, asilimia 47 wavulana na asilimia 10 ni walemavu wenye umri wa miaka 15-35 na wameshaanza mafunzo ya ufundi stadi mwezi huu katika vyuo vya Veta na mashirika 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!