Mwanahabari na blogger wa mtandao wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika geti kuu la kuingilia katika ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa zilizopo eneo la Mang'ula, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, Tanzania. Alipokuwa katika habari za Utafiti jinsi ya Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri mbuga na hifadhi za Taifa nchini (How Climate Change Effect The National Parks in Tanznia) hivi karibuni (Picha na modewjiblog).
Na Andrew Chale, modewjiblog
[TANZANIA] Zimebaki siku zaidi ya 60, kuelekea mkutano mkuu wa 21 (COP21) wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Nchi (UNFCCC) unaotarajiwa kufanyika Paris, Ufaransa. mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Dulu na chunguzi za kitafiti zinaeleza kuwa, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa Barani Afrika yatakayokumbwa na janga kubwa dhidi ya Mabadiliko ya tabianchi (Climate Change in Tanzania National Parks) kwenye Hifadhi na mbuga zake.
Dulu hizo za kitafiti pia zinabainisha kuwa, asilimia kadhaa za Wanyama nao watatoweka kabisa hali ambayo taifa litakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kushuka kwa uchumi wa Nchi katika siku za usoni.
Hivi karibuni, mwandishi wa Makala haya wa modewjiblog, alipata kutembelea Hifadhi kadhaa za taifa zilizo chini ya usimamizi wa Shirika la Hifadhi la Taifa, Tanzania National Parks Authority (TANAPA). Hifadhi hizo zikiwepo Udzungwa, Selous Game Reserve, Mikumi, Ruha, na Saadan pamoja na kuonana na wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi kwenye idara za serikali na watu binafsi.
Eneo la kuingia katika Hifadhi na makao makuu ya hifadhi ya Udzungwa...
Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa:
Kwa mujibu wa tovuti ya Serikali inabainisha kuwa Udzungwa ni miongoni mwa milima yenye Bionuwai nyingi iliyozungukwa na misitu.
Hata hivyo vyanzo mbalimbali vinabainisha kuwa, Hifadhi hii ya Udzungwa ni miongoni mwa Hifaadhi zilizo kwenye hatari ya kutoweka kutokana na mipango hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Vyanzo vya ndani vinaeleza kuwa, ili kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabianchi yasiathiri Hifadhi hizo, juhudi za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwemo wasimamizi na wananchi wanaozunguka hifadhi kupewa elimu ya kutosha pamoja na mipango kazi ya mara kwa mara.
Bwana Ruombano Mnege (56) mkazi wa kijiji cha Msolwa katika eneo jirani na hifadhi ya Udzungwa anaeleza kuwa, afahamu maana ya mabadiliko ya tabianchi, ila anachoelewa ni kuwa mambo yanabadilika pindi Mungu anapoamua.
"Mimi natambua Mungu anapoamua ndio mambo yanatokea. Suala la mabadiliko ya tabianchi kwa sie wa huku hasa wakulima hatutambui sana kwa sababu hatuna elimu ya kutosha” alibainisha Mnege akijibu maswali endapo wasimamizi wa hifadhi hizo kama wanawashirikisha wananchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hata hivyo, wakazi wengi wa maeneo ya jirani na hifadhi wanabainisha kuwa, hawana elimu ya kutosha katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hali inayowapa hofu kukumbwa na janga hilo la ukame siku za usoni.
Ambapo walibainisha kuwa, wapo watu wasio waaminifu wakiingia katika hifadhi hizo na kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji, kuchoma moto misitu pamoja na kuwinda wanyama.
"Kulikuwa na wanyama wakifika hadi kwenye mashamba yetu miaka ya nyuma. Lakini kwa sasa wanyama wale hawafiki kabisa kutokana na hali ilivyo huenda wamepotea” anaeleza Bi. Jonesia Simon mkazi wa Sanje ambapo anasema kutoonekana kwa wanyama hao kwa hivi sasa kumechangiwa na mabadiliko ya tabianchi kwani kulikuwa na wanyama waliokuwa wakifuata maji na wengine walikuwa wakifuata vyakula kwenye mashamba hayo lakini kwa sasa wametoweka kabisa.
Mwandishi wa makala haya, Andrew Chale wa modewjiblog.com akiwa katika eneo la Sanje wakati wa kupanda mlima Udzungwa kuelekea kwenye maporoko ya Udzungwa (Picha na modewjiblog team).
ramani inayoonyesha hifadhi hiyo ya Udzungwa..
Milima ya udzungwa ni jina la hifadhi inayopatikana hifadhi hiyo ndani ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro pamoja na upande wa Iringa. Milima hii ni makazi ya wanyama pori wa aina mbalimbali huku ikiwa na ukubwa wa kilometa 1990.
Udzungwa ni miongoni mwa hifadhi zenye hazina ya aina nyingi za mimea, ndege na wanyama ambao hawapatikani katika sehemu nyingine duniani.
Hifadhi iko umbali wa kilometa 350 kusini mwa Dar es Salaam, kilometa 65 kutoka katika Hifadhi ya Mikumi ambayo ni ya jirani kabisa.
Kati ya aina sita za jamii ya nyani wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni : Mbega Mwekundu, wa Iringa (Iringa red colobus monkey) na aina ya pili ni Sanje Crested mangabey.
Huku kukiwa na aina mbalimbali za ndege na aina nne za ndege ambao hazikufahamika hadi katika miaka ya karibuni. Ndege ni Chozi bawa jekundu (rufous-winged sunbrid) na wengine wengi akiwemo kwale Udzungwa.
Hifadhi hii pia ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani Afrika.
Picha ya juu Maporoko hayo na chini ni Mwandishi wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa wakati alipotembelea kuandika habari za Mabadiliko ya Tabianchi namna yanavyoweza kuathiri Hifadhi za Taifa nchini. (Picha na modewjiblog team).
Mwandishi wa makala haya wa modewjiblog.com, Andrew Chale akiwa katika eneo la awali na mapumziko baada ya safari ndefu ya kupanda mlima huo katika kuelekea kwenye maporomoko hayo ya Udzungwa (Picha na modewjiblog team).
Maporomoko ya Sanje:
Ndani ya hifadhi hii pia ina Mto Sanje ambao ni kivutio kikubwa sana. Mto huu una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni.
Hata hivyo, mbali na kuwa na vitu vyote hivyo ndani ya hifadhi hii ya Udzungwa, Serikali na jamii inayozunguka hiafdhi hii inawajibu mpana wa kukabiriana na mabadiliko ya tabianchi kwani wasipochukua hatua vitu hivyo vinaweza kutoweka na nchi ikaja kukosa mapato kwani Utalii ni miongoni mwa sekta inayoiingizia Tanzania fedha nyingi za kimaendeleo.
Wanyama kutoweka:
Tovuti ya Serikali ya Makamu wa Rais (http://www.vpo.go.tz/news), imebainisha kuwa: Inakadiriwa kwamba asilimia 34 ya ardhi ya Bara la Afrika iko katika hatari ya kugeuka jangwa kutokana na mabadiliko ya TabiaNchi.
Na kuongeza kuwa: Hali hii ya mabadiliko ya TabiaNchi itachangia kutoweka kwa asilimia kati ya 25 hadi 40 ya aina fulani za wanyama katika hifadhi Barani Afrika ifikapo mwaka 2020 na kwamba maeneo kame yataongezeka kwa asilimia 5 hadi 8 Barani Afrika ifikapo mwaka 2080.
Msemaji wa TANAPA:
Hata hivyo suala la mabadiliko ya tabianchi katika hifadhi za Taifa nchini bado halijapewa kipaumbele kikubwa hasa kwa wadau wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo wanahabari, wanaharakati wa mazingira na wananchi wanaoishi jirani na hifadhi. Hii inatokana na hata wakati mwingine kukosa ushirikiano wa karibu kutoka kwa mamlaka husika ikiwemo makao makuu ya ofisi za TANAPA ambao ndio wenye jukumu la kutoa taarifa za kina kitaalamu.
Mwandishi wa makala haya akiwa katika view point ya maporomoko hayo..
Taswira ya eneo la maporomoko ya Udzungwa inavyoonekana unapokuwa katika eneo la awali la View Point ndani ya Hifadhi hiyo ya Udzungwa. Katika taswira hiyo panaonekana kama ramani ya Afrika. (Picha na Andrew Chale,modewjiblog).
eneo la maji yanayotoka kwenye maporomoko hayo ambapo kwa kipindi hiki yanapoonekana yakiwa yamepungua kutokana na kipindi maalum. Hata hivyo maji hayo kuna msimu yanajaa zaidi ..
Miongoni mwa aina za ndege wanaopatikana ndani ya hifadhi hizo za Udzungwa ambapo inaelezwa kuwa Hifadhi hiyo imekuwa ikitembelewa na ndege mbalimbali kutoka maeneo mengi ya nchi za Afrika.
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya misitu hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Miongoni mwa miti inayopatikana ndani ya Hifadhi hiyo ambayo hata hivyo bado inakabiriwa na changamoto kwa watu wasio na mapenzi mema kuvamia na kukata miti hiyo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za mbao na mambo mengine.
Miongoni mwa miti ambayo inapatikana ndani ya hifadhi hiyo ambayo ni dawa na pia ni miongoni mwa miti inayopendwa na wanyama hata hivyo ipo katika changamoto ya kutoweka...
Red Col wanaopatikana ndani ya Misiti hiyo ya Hifadhi ya Udzungwa..
Mwandishi wa makala haya wa modewjiblo, Andrew Chale akiwa katikati ya Hifadhi hiyo wakati wa kuyatafuta Maporomoko hayo. Ambapo ndani ya msitu huo wenye baridi muda wote kutokana na kuzungukwa na miti mbalimbali.
Misitu hiyo ya Udzungwa inavyoonekana..
Itaendelea ripoti sehemu ya Pili…
Ripoti hii imeandaliwa na Andrew Chale, Mwandishi wa Habari na Mhariri wa mtandao (blog) ya modewjiblog.com ya nchini Tanzania. ( Anuani : +255719076376 au barua pepe: andrewchale@gmail.com).
Makala haya yamefadhiliwa na kwa ufadhili wa Shirika la ( CFI) la nchini Ufaransa, chini ya mradi wa Medias 21 Africa & Asia.
No comments:
Post a Comment