Friday, 30 October 2015

TANGAZO- NAFASI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA- SHULE ZA SEKONDARI WAMA NAKAYAMA NA WAMA SHARAF

New Picture (6)Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama, Nyamisati -Rufiji


New Picture (5)
Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf, Mitwero Lindi
New Picture (7)
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha kwanza kwa wasichana katika Shule zake mbili za Sekondari:
(1) Shule ya Sekondari WAMA – Nakayama iliyopo Kijiji cha Nyamisati Wilaya ya Rufiji , Mkoa wa Pwani:
(2) Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero katika Manispaa ya Lindi
WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inaendesha shule hizi maalum kwa ajili ya watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Hata hivyo, WAMA inatoa fursa chache kwa wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia ili kuongeza uwezo wa kusaidia watoto wengi zaidi.
Tunafurahi kutoa fursa hii kwa wasichana ambao wataweza kulipia ada kwa kidato cha kwanza katika shule zote mbili kwa mwaka 2016.
Fomu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam zilizopo Kawe karibu na Hoteli ya Picolo Beach au katika Tovuti ya Taasisi: www.wamafoundation.or.tz
Kwa wakazi wa Lindi fomu zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la Lindi zilizopo katika makutano ya Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na Ofisi za Magereza za Mkoa wa Lindi
Kwa Dar es Salaam mtihani wa kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba 12, 2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani.
Kwa Lindi mtihani wa kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba 19 , 2015 katika Chuo cha VETA Lindi.
Mwanafunzi anatakiwa arudishe fomu pamoja na risiti ya malipo katika ofisi za Taasisi ya WAMA au kwa kutumia barua pepe: info@wamafoundation.or.tz, mbugunimwajuma@gmail.com na alimindria66@yahoo.com. Mwisho wa kurudisha fomu ni Jumatano tarehe 11 Novemba, 2015.
Shule zetu zina mazingira na huduma zote muhimu zinazowawezesha wanafunzi kufaulu vizuri yakiwemo mabweni ya kisasa, maabara za kisasa, maabara za computer, maktaba zenye vitabu vya kutosha na walimu wazuri na wakutosha.
Kwa Mawasiliano zaidi:
Piga Namba: 0685-651449, 0789-000341, 0754-439183,
Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz
Tovuti: www.wamafoundation.or.tz

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!