Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeviomba vyama vya siasa kutumia majukwaa ya siasa katika kipindi hiki kifupi kuelezea sera za vyama vyao ili kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi na kuepuka lugha za uchochezi zinazoweza kuhatarisha maisha ya watanzania.
Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi Profesa Amon Maligha amelazimika kutoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Mtwara.
Amesema tume imeanza kushuhudia uvunjifu wa maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni ikiwa ni pamoja na lugha za uchochezi na kejeli zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa kuepuka kushawishi ama kuhamasisha mambo yanayoweza kuvuruga amani.
Kwa upande wake msimamizi wa tume ya uchaguzi kanda ya kusini Grecensia Mayala amesema vifaa vya uchaguzi vimekuwa vikiingia katika mkoa wa Lindi na Mtwara kwa awamu na hivi sasa mikoa hiyo imeanza kupokea karatasi za kupigia kura na kusafirishwa katika majimbo
CHANZO:ITV.
No comments:
Post a Comment