Monday, 19 October 2015

Mwili wa kijana aliyezama maji na gari kivuko cha Kigamboni umeonekana eneo la Ocean Road.

Mwili wa kijana Odva Makenge aliyezama maji baada ya gari walilokuwa wamepanda ndani ya kivuko cha kigamboni kutumbukia baharini umeonekana kando ya bahari ya Hindi eneo la Ocean Road huku famili ya marehemu ikilalamikia polisi kikosi cha wanamaji kwa kushindwa kuchukuwa hatua haraka.



Wakizungumza na ITV wakiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambako mwili wa marehemu umepelekwa kwa uchunguzi ndugu zake wamesema walikuwa wameamua kufanya jitihada binafsi kutafuta wazamiaji na kuitaka serikali kuwachukulia hatua wafanyakazi wa kivuko kwa kushindwa kusimamia sheria za ndani ya pantoni pamoja na kukaa kimya baada ya tukio.
 
Akijibu malalamiko hayo kamanda wa kikosi cha wanamaji Mboje Kanga amesema mtoa taarifa alipeleka taarifa polisi wa kikosi cha usalama barabarani badala ya kikosi cha wanamaji hivyo kuchelewa kwa taarifa kumechangia wao kuchelewa kuchukuwa hatua na kueleza jitihada walizofanya katika kuutafuta mwili huo.
 
Gari lililohusika na tukio hilo lina namba za usajili T252 CFW aina ya Toyota Marck two ambalo bado halijaonekana na dereva anashikiliwa na polisi kikosi cha wanamaji kwa mahojiano na chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni ulevi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!