Thursday, 22 October 2015

MGWIRA AAHIDI KUSIMAMIA MAPATO YA KODI KUPUNGUZA MASIKINI

Mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Anna
Tarime. Mgombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Anna Mghwira, amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuingia madarakani atahakikisha anasimamia ukusanyaji kodi ili kupunguza gharama za maisha na kupambana na umasikini.


Mghwira ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa mpira Serengeti Jimbo la Tarime Mjini, huku akiwanyooshea kidole wenye makampuni makubwa ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya makampuni yao na mzigo huo kubebeshwa wananchi masikini.
Amesema matatizo hayawezi kuisha kwa kukwepa kulipa kodi, huku serikali ikiwa na mzigo mkubwa wa deni la taifa ambalo badala ya kulitafutia ufumbuzi kwa kusimamia misingi imara ya ukusanyaji kodi, badala yake linaongezwa kila kukicha kwa kukopa fedha zisizowasaidia wananchi , huku makampuni makubwa yakisamehewa kodi.
Ameeleza kuwa serikali yake itafumua mikataba yote ya madini, sekta ya utalii, gesi asilia na kuiangalia upya ikiwamo kuweka uwazi na wananchi wafahamu kila kinachoendelea katika rasilimali za nchi.
"Gesi asilia, utalii na madini matumizi yake yameanishwa kwenye ilani ya chama kuwa itakuwa mali ya wananchi kikatiba, hakutakuwa na ubabaishaji katika hilo wala kodi za wananchi" amesema Mghwira.
Amesema kwa miaka 50 hakuna anayefahamu kodi za nchi zimefanyiwa nini, zaidi ya kusikia sifa za ujenzi wa mabarabara, madaraja ambayo pembeni kuna mabango makubwa yakieleza kuwa zimejengwa kwa msaada wa Wamarekani na Wachina.
Amefafanua kuwa CCM imesimamisha mgombea dhaifu ambaye anashangaa kila kitu huku akiwa ndani ya Serikali hiyo anayoishangaa kwa kushindwa kutimiza wajibu wake

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!