Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akimpigia kampeni mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi, Dk. Harrison Mwakyembe. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna akihutubia wakazi wa Wilaya ya Kyela katika mikutano ya Kampeni |
Paul Makonda akiwanadi wagombea udiwani wa Kata mbali mbali za Jimbo la Kyela |
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akimuombea Kura Dk. Mwakyembe. |
WATUMISHI wawili wa Shirika la Umeme(TANESCO) Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuondoka wilayani hapa kwa tuhuma za kuhujumu huduma za jamii zinazofanywa na Serikali ikiwemo miradi iliyoanzishwa na Dk. Mwakyembe.
Watumishi hao ambao ni Meneja wa Tanesco na Mhasibu wake Wilaya ya Kyela (majina hayakupatikana) wanatuhumiwa kukata umeme katika visima vya maji ili wananchi wakose huduma ya maji.
Hayo yalibainishwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alipokuwa akimuombea kura Dk. Harrison Mwakyembe katika kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kyela jana.
Makonda alisema zipo taarifa kwamba watumishi hao walikuwa wakikata umeme kwa maksudi ili ionekane Kyela kuna uhaba wa maji na Mbunge aliyekuwepo Dk. Mwakyembe ameshindwa kufanya kazi jambo ambalo sio kweli.
“Ndugu zangu wanaKyela naomba ni waambie ukweli kwamba zipo njama za maksudi za kumdhoofisha Dk. Mwakyembe kwa watumishi hawa wa Tanesco kukata umeme wa maksudi kwenye visima ili visitoe maji sasa nawatangazia kuwa hawa watumishi watahamishwa mara moja” alisema Makonda.
Alisema Dk. Mwakyembe alikwisha chimba visima viwili vyenye uwezo wa kutoa ujazo wa mita 90 na 91 lakini bado maji hayo hayatoshelezi mahitaji kutokana na ongezeko la watu hivyo anampango wa kutanua visima hivyo hadi kufikia ujazo wa mita 1500 na kuendelea.
Aliongeza kuwa mbali na hujuma zilizofanywa na watumishi hao wa Tanesco pia wapinzani wa Dk. Mwakyembe wamemwaga fedha jimboni hapo ili kuhakikisha Mwakyembe hashindi uchaguzi huu.
Alisema lengo la fedha hizo ni kuhakikisha Mwakyembe haingii Bungeni ili wao waendelee na ufisadi wao kwani wamemuona Mwakyembe kama mwiba mkali kwao kwa kukemea ufisadi wazi wazi.
“Kuna frdha nyingi zimemwagwa ili kuhakikisha Mwakyembe hapiti mimi niwaambieni chukueni hizo fedha ili zisaidie kumuongezea kura Mwakyembe pamoja na Magufuli” alisema Makonda.
Alisema Dk. Mwakyembe anamikakati mingi ya kuhakikisha Kyela inakuwa vizuri kiuchumi ambapo hivi sasa ana mipango ya muda mfupi, kati na Muda mrefu ya kuanza kujenga meli tatu kubwa.
Alisema mbali na meli pia Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa ushirikiano na Jeshi la Wananchi wanatarajia kuanza kujenga uwanja mdogo wa ndege kwani mazungumzo yako katika hatua nzuri.
Aidha aliwasihi wakazi wa Wilaya ya Kyela kumpigia Kura za ndiyo Mgombea Urais John Magufuli na kumkataa Edward Lowasa kwa kile alichodai hafai kuwaongoza watanzania kutokana na kashfa alizonazo.
Alisema Lowasa ni fisadi namba moja nchini kwani Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa wa Kwanza kumkataa mwaka 1995 kwa tuhuma za ufisadi pia anatuhumiwa kwa migogoro ya Tanesco, kupora lanchi ya taifa pamoja na kuzungumza uongo majukwaani.
Alisema Lowasa ni kigeugeu kwani alipokuwa akitanga nia Arusha alisema Kikwete kafanya mambo mengi mazuri hivyo akiingia yeye atayaendeleza lakini baada ya kuhama ameanza kusema Kikwete kaharibu uchumi jambo ambalo linaonesha kuwa hafai kabisa.
Alisema tatizo linguine ni kutumia udini na ukabila kutaka kuingia madarakani jambo ambalo linaweza kuhatarisha umoja na mshikamano wa Watanzania na kwamba kundi linalomsaidia sasa ni kundi ambalo liliondolewa madarakani kwa kashfa.
“ Hebu fikiria watu waliokataliwa na Watanzania eti ndiyo walionyuma yake kama akina Rostam na Kalamagi wao waliondolewa madarakani kwa sababu walikuwa hawafai kuongoza leo wanamsaidia huyu pia hatufai wala msimchague” alisema Makonda.
Aliongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mrahisi kuliko chaguzi zingine kwa sababu unashindanisha pande mbili ambazo moja inaongozwa na Dk. Magufuli ya uadilifu, utendaji na kujali Watanzania na upande wa pili ukiongozwa na Lowasa ambaye ni Fisadi, mwizi, mkabila na siyeitakia mema Tanzania.
“Nimalizie kwa kunukuu maneno ya Biblia ambayo yanasema unanafasi mbili na unatakiwa kuchagua moja umauti au Uzima pimeni wenyewe” alisema Makonda.
No comments:
Post a Comment