Wednesday, 21 October 2015

FAIDA 20 ZA MAZOEZI YA KUTEMBEA

Kutembea ni njia salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na maradhi. Mazoezi au tabia ya kufanya mazoezi inayo faida kubwa zaidi kuliko matumizi ya dawa.
Faida 20 za Mazoezi ya Kutembea


1. Mazoezi husaidia kupunguza uzito, tembea lisaa limoja kila siku
2. Ni mazoezi yanayoweza kufanywa na kila mtu
3. Ni mazoezi yasiyohitaji vifaa/hayana gharama
4. Ndiyo njia rahisi kabisa ya kuufanya mwili kuwa mkakamavu
5. Hupunguza dalili za majonzi na wasiwasi
6. Ni mazoezi yenye matokeo ya taratibu
7. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kolesto/lehemu
8. Hupunguza na kutibu shinikizo la damu
9. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi za kansa
10. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
11. Hukufanya ujisikie vizuri
12. Husaidia kuimarisha mifupa
13. Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na shambulio la moyo
14. Ni mazoezi uwezayo kuyafanya bila kukusababishia ajari au maumivu makubwa
15. Hupunguza mfadhaiko/stress
16. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo
17. Ni mazoezi unayoweza kuyafanya bure bila kulipia chochote
18. Husaidia kuimarisha mishipa
19. Husaidia katika mfumo wa upumuwaji
20. Husaidia kuongeza mzunguko wa damu
Kama afya yako siyo nzuri sana anza kutembea kidogo kidogo labda dakika 10 kwa siku huku ukiongeza dakika 5 kila siku hadi hapo utakapoweza kutembea lisaa limoja mfululizo bila kupumzika. Ili kupunguza uzito, unene, utipwatipwa, mafuta yaliyozidi au kitambi, fanya zoezi la kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo muda wa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo.
Je ni muda gani mzuri wa kufanya mazoezi ya kutembea?,
Wengi wanapenda asubuhi sana na jioni lakini mimi napenda kufanya mazoezi ya kutembea mchana wakati wa jua kali saa sita, saa saba au saa nane. Utanishangaa kwanini nafanya hivi!, Jua lina umhimu sana kwa afya ya mwili na ngozi pia kama chanzo cha vitamini D, vitamini ambayo ni mhimu sana katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis), kuzuia maumivu ya mishipa, kushusha shinikizo la damu, Kudhibiti kisukari, kudhibiti kolesto na kadharika.
Unapotembea mchana wa jua kali unaruhusu jua kutua juu yako mwili mzima.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!