Tuesday 27 October 2015

KIGOGO WA MADAWA YA KULEVYA MBARONI


KIGOGO wa biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, mkazi wa Kinondoni, Dar, Fred William Chonde amefungwa jela miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 akitoka baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na unga.

Kigogo wa biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’, mkazi wa Kinondoni, Dar, Fred William Chonde.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa zinasema, Chonde alihukumiwa Septemba 2, mwaka huu na Jaji Edson Mkasinongwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Kamanda Nzowa alisema kwamba, wakati Chonde akihukumiwa, mwenzake aliyejulikana kwa jina la Kambi Zuberi aliachiwa huru kwa kutoonekana na kosa.
“Naipongeza mahakama kuu kwa sababu majaji kwa sasa wamekuwa makini katika kesi za madawa ya kulevya na wamekuwa wakizishughulikia na kutoa maamuzi haraka. Siyo katika kesi hii tu bali zipo nyingi ambazo hukumu zimeshatolewa na wahusika kufungwa jela.
Mzigo wa unga aliodaiwa kukutwa nao.
“Unajua zamani kesi zilikuwa zikirundikwa na kuchukua muda mrefu bila kusikilizwa lakini kwa sasa kuna jitihada kubwa zinazofanywa na majaji na hii inatoa hofu hata kwa wananchi ambao walikuwa na fikra tofauti na serikali yao juu ya wafanyabiashara wa unga,“ alisema Nzowa.
Chonde alikamatwa na polisi wa kitengo cha madawa ya kulevya, Februari 21, 2011, Tegeta Jogoo, Dar wakiwa na kilo 180 aina ya heroin yenye thamani ya shilingi bilioni 5.2.
Chonde alikamatwa na wenzake watatu, Kambi Zuberi na Wazungu Shahaz Marik na Abdul Ghan ambao ni raia wa Afrika Kusini. Waliwekewa dhamana lakini inasemekana walitoroka nchini na katika siku zote za kesi yao hawajawahi kuonekana mahakamani

CHANZO:GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!