Monday 26 October 2015

JOYCE KIRIA : KWANINI MUME WANGU AKATALIWE KUHESABIWA KURA ZAKE?



Jimboni Mwanga Kilimanjaro; am real sad!
Tangu asubuhi Mgombea ubunge wa Chadema My Hubby Kilewo, anataka warudie kuhesabu zile karatasi za kura kutokana na dosari walizokumbana nazo kwenye majumuisho! Lakini wasimamizi wamekataa katakata! Yaani toka asubuhi wanawaomba warudie kuhesabu lakini hawataki... kwanini??? Jamani wadau wa uchaguzi hii ni Haki kweli??? Kwanini wasirudie kuhesabu ili mgombea ajiridhishe???

Aidha Mgombea mwenzake Magembe anamshinikiza Mkurugenzi kutangaza matokeo ambayo yana ukakasi.
Mbaya zaidi huyo mkurugenzi anakubaliana na huyo Magembe! Inaumaaaaaaa

Ivi kama mgombea hana imani na kura zake kutokana na sababu kadhaa zikiwepo za mawakala kumuhujumu, na ushahidi upo wazi wazi, kwa kubadilisha kura zake katika baadhi ya karatasi za matokeo, mgombea Akitaka warudie kuhesabu haruhusiwi???? Kwa nini mume wangu amekataliwa kuhesabiwa upya kura zake???? Haki ya mgombea iko wapi?????
Vinginevyo mabomu yamepigwa kutawanyisha watu waliokuwa wanadai Haki itendeke ili wajiridhishe kama kweli wanajua hawajafunga goli la mkono!!!!!
(Aisee Ile ndoto ya Nyumba nzuri na shoping za vitu vizuri ulaya naona ikififia Chaaaa 😭😭😭😭 Tena vijisent vyetu na michango juu navyo kwishaaaaa! Jamani siasa ni mgodi aisee, unameza pesa niaje? Yeeesu! Halafu hujui mgodi wenyewe utatema mawe lini? Nikiangalia vipesa vilivyoishia hapa roho inaumajeeee???)
Nafwaaaaaaaaaaa
Kwa sasa naumwaaaaa sanaaaàa😷😷😷😷 nishatumia 💉💉💉💉💊💊💊🍻🍻🍻🍻🍻 ilimradi nisiyasikie maumivu lakini wapiiii! yakipungua nitarudi😩😩😩
Lakini naomba kushukuru kwa wale wote waliotuunga mkono kwa hali na mali mpaka hapa!
Ameen🙏🙏🙏🙏

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!