Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Maiko Bundala (26) Mkazi wa Kijiji cha Mnyagala Wilaya ya Mpanda kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto (8) na kumuharibu vibaya katika sehemu zake za siri
Hukumu hiyo iliyovutia hisia za watu wengi wa Mji wa Mpanda ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo wa upande wa mashitaka na utetezi.
Awali katika kesi hiyo Mwanasheria wa Serikali Kulwa Kusekwa alidai mahakamani hapo kuwamshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Machi 27 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni
Siku hiyo mtoto huyo aliyebakwa alikuwa akicheza katika eneo la nyumba ya mshitakiwa huku akiwa na watoto wenzake wa eneo hilo
Alidai kuwa ndipo Bundala alipowatuma watoto waliokuwa wakicheza na mtoto aliyembaka wakanunue pipi dukani na yeye alibaki na mtoto huyo
Alieleza kuwa baada ya kuona amebaki na mtoto huyo alimwingiza ndani ya chumba chake na kisha alimvua nguo kwa nguvu huku na kisha alianza kumbaka huku akiwa amemziba mdomo iliasipige kelele
Katika ushahidi alioutowa Mahakamani hapo mama wa mtoto aitwaye Sofia Masanja aliiambia Mahakama kuwa siku hiyo ya tukio mtoto wake alikuwa akicheza katika eneo la nyumba ya mtuhumiwa huku akiwa na watoto wenzake
Alidai kuwa baada ya kuona mtoto wake amechelewa aliamua kumfuata alikuwa akicheza na wenzake na alipofika kwenye nyumba ya Bundala alikuta wale watotowote hawapo na alisikia mtoto akilia hivyo hakujua kama ni mtoti wake
Alieleza kuwa baada ya muda mfupi mtoto wake alirudi nyumbani huku analia na alimweleza Mama yake kuwa Bundala amemuingizia sehemu zake za siri na amemuumiza kwenye sehemu zake za siri hari ambayo ilimfanya mama wa mtoto huyo kuanza kulia huku akielekea kwa mtendaji wa Kijiji
Baada ya kufikishwa kwenye uongozi wa Kijji mshitakiwa alikana kumbaka mtoto huyo na ndipo walipoamua mshitakiwa afikishwe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda
Shahidi wa tano wa kesi hiyo ambae ni daktari alidhibitisha Mahakamani hapo kuwa vipimo alivyofanyiwa mtoto huyo vilionyesha kuwa mtoto huyo alikuwa ameingiliwa katika sehemu zake za siri na kuharibiwa
Katika utetezi wake Mahakamani hapo mshitakiwa aliomba Mahakama imwachie huru kwani yeye hakutenda kitendo hicho isipo kuwa alikuwa anakuwa akimdai fedha mama wa mtoto huyo ndio maana aliamua kumsingizia kuwa amembaka mtoto wake
Baada ya utetezi huo ambao ulipingwa vikali na Mwanasheria wa Serikali Kulwa Kesekwa na aliiomba Mahakama itowe itowe adhabu kali kwa mshitakiwa kwani tabia ya kuwabaka watoto wadogo inaonekana kushamiri katika Wilaya ya Mpanda
Hakimu Chiganga baada ya kuzisikiliza pande zote mbili za utetezi na mashitaka aliiambia Mahakama kuwa Mahakama bila shaka yoyote imetia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kuvunja sheria no 130(1) (2)k na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002
Hivyo kutokana na kosa hilo Mahakama imemuhukumu Maiko Bundala kutumikia jela kifungo cha maisha jela kuanzia jana
No comments:
Post a Comment